STAMICO KUJA NA NISHATI YA MAKAA YA MAWE KWA MATUMIZI YA MAJUMBANI,VIWANDANI - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

STAMICO KUJA NA NISHATI YA MAKAA YA MAWE KWA MATUMIZI YA MAJUMBANI,VIWANDANI

Share This
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

SHIRIKA la Taifa la Madini (Stamico) limesema makaa ya mawe yakianza kutumika kama nishati ya kupikia kutapunguza matumizi ya mkaa kwa asilimia 15.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Madini na huduma za Kiuhandisi, Zena Kongoi wakati akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Mazingira Dunia yaliyohitimishwa, leo Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam amesema Stamico katika miradi mbalimbali wameweka kipaumbele cha utuzaji wa mazingira katika kulinda vizazi vya leo na vijavyo.

Amesema kuwa katika ripoti ya Trido inaonyesha hekta 300,000 za miti zinakatwa kwa ajili mkaa hivyo matumizi ya makaa ya mawe kutumika nishati ya kupikia itapunguza ukataji wa miti hiyo.Kongoi amesema makaa ya mawe kuna taasisi ambazo zitakuwa za kwanza kufikiwa na nishati ya makaa ya mawe ni Magereza , Kambi za Wakimbizi pamoja na vyuo vikuu.

Amesema kuwa nishati hiyo watauza kati ya Sh.350 hadi 500 ambapo kila mtu anaweza kumudu na kuachana na matumizi ya mkaa kutokana na gharama iliyopo katika mkaa.Amesema majaribio ya makaa ya mawe yana gesi hivyo kazi kwa ushirikiano kati ya Stamico na Trido katika kutoa gesi hiyo na kemikali zingine zilizo katika makaa ya mawe.

Kongoi amesema stamico iko bega kwa bega na wadau mbalimbali katika shughuli za madini katika kuangalia masuala ya mazingira ikiwemo kufanya tathimini ya uhalibifu wa mazingira katika miradi.
Kaimu Mkurugenzi wa Madini na huduma za Kiuhandisi, Zena Kongoi akizungumza na waandishi habari katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria wa Baraza la Mazingira (NEMC), Heche Suguta akiwapa vipeperushi pamoja na kuwapa maelezo wananchi waliotembelea maonesho ya wiki ya mazingira katika viwanja vya Mnazi Mmoja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad