SEKTA YA UFUGAJI SAMAKI INAKUA, ITASAIDIA KUONGEZA KIPATO-ULEGA - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

SEKTA YA UFUGAJI SAMAKI INAKUA, ITASAIDIA KUONGEZA KIPATO-ULEGA

Share This

Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema sekta ya ufugaji samaki inakua na inasaidia katika kuongeza ajira na kipato kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla na hiyo ni kutokana na ubora wa samaki wanaozalishwa nchini.

Ulega ametoa kauli hiyo leo alipofanya ziara ya kutembelea Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Mbegani, shamba la ufungaji wa samaki la NFCO Ruvu,Ruvu fish farm Mlandizi,Kiwanda cha kuzaliza chakula cha kuku na samaki,Hill feeds Mapiga,wakulima wa Mwani Bagamoyo Milingotini.

Aidha amesema vijana wengi wanamaliza vyuo na kukosa ajira, hivyo wataboresha sekta hiyo ili kuongeza ajira kwani biashara ya samaki inalipa na kwa kasi iliyopo Taifa na wananchi watapata kipato kikubwa.

Akizungumzia kuhusu kutopatikana kwa vifaranga Ulega ameeleza wamejipanga katika kutatua tatizo hilo hasa katika kuhakikisha uzalishaji unaongezeka katika vituo vya uzalishaji wa vifaranga vya samaki kama Luhila Songea na Nyegezi mkoani Mwanza.

Pia amesema changamoto ya chakula cha samaki imetatuliwa na baada ya kutembelea kiwanda cha chakula cha Hill Package kilichopo Mpinga Bagamoyo ameridhika na utendaji na uzalishaji wa chakula cha samaki katika kiwanda hicho. Hivyo amewashauri wafugaji kutumia chakula kutoka katika kiwanda hicho kinachomilikiwa na wazawa na badala ya kuagiza chakula kutoka nje ya nchi.

Ametoa mwito kwa wananchi kushirikiana na Serikali kutokomeza uvuvi haramu ili kuongeza kipato kwa wavuvi na taifa kwa ujumla. 
 Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia akiangalia sabuni pamoja na mafuta ya kupaka yanayotengenzwa na zao la Mwani katika kijiji cha Bagamoyo mkoa wa Pwani.
 Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega (kulia) akimsikiliza Mmiliki wa Shamba la kufugia samaki,Khumbo Kathenga
 Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega (katikati) akiangalia vyakula vya kuku na samaki vinanyo zalishwa na kiwanda cha  Hill feeds kilichopo Mapiga mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega (kushoto) akizungumza na wamiliki wa shamba la samaki lilipo Ruvu mkoa wa Pwani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad