RC KAGERA -VIONGOZI WA WILAYA WATOE USHIRIKIANO KUTAMBUA VIKUNDI ILI WANUFAIKE NA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII(NSSF) - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

RC KAGERA -VIONGOZI WA WILAYA WATOE USHIRIKIANO KUTAMBUA VIKUNDI ILI WANUFAIKE NA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII(NSSF)

Share This
Na Editha Karlo wa blog ya Jamii Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera amewataka viongozi wote wa Wilaya kuhakikisha wanatoa ushirikiano katika kutambua vikundi vyote katika maeneo yao ili Mfuko wa Hifadhi ya jamii Taifa (NSSF) waweze kuwafikia na kuweza kuingia katika mpango wa hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu katika ufunguzi wa semina juu ya mpango wa hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi.

"Maafisa biashara na maafisa ushirika natambua mnazo orodha za vikundi vyote vilivyopo kuanzia ngazi ya Wilaya hadi Mkoa niwaombe muwapatie hizo orodha NSSF na muwaunganishe na vikundi husika ili waweze kuwafikia wote na kuwapa elimu ya manufaa yanayopatikana iwapo watakuwa wanachama wa NSSF"alisema

Kinawilo aliwataka viongozi wote wa vikundi waliohudhuria semina hiyo kuhakikisha ujumbe unawafikia wale wanaowaongoza na kuandaa mazingira ambayo yatawawezesha kufikiwa na NSSF kwaajili ya kunufaika nayo.Alisema wajasiriamali wengi wamekuwa na kilio cha mitaji,na mara nyingi wanapoomba mikopo wanapewa kwa riba za juu kiasi cha kuwafanya washindwe kupata faida inayositahili na kushindwa kuendelea.

"Nimeelezwa mpango huu wa hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi hasa kwa wanachama wa saccos na waliojiunga NSSF ambao wapo katika vikundi vyenye sifa husika wanaweza kukopeshwa kupitia usimamizi wa benki ya Azania na NMB tunaomba mtoe mikopo kwa riba nafuu na kwakuwa wahusika mpo mtaje kiwango cha riba wazi hapa"alisema

Mariam Muhaji Mwenyekiti wa kamati ya kuratibu sera ya hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi alisema kuwa serekali ya awamu ya tano ni serekali inayomjali kila mtu hasa watu wa hali ya kipato cha chini,kwa kutambua umuhimu huo bunge limeshapitisha sheria mpya namba 2 ya mwaka 2018 inayoboresha hifadhi ya jamii nchini ambapo sheria hiyo imeacha mifuko miwili ambayo ni PSSSF na NSSF.

Alisema mpango huo una manufaa mengi ikiwemo kugharamia matibabu,kinga za majanga,pensheni za uzee mafao ya uzazi na mafao mengine muhimu.

"Tunafahamu zamani swala la hifadhi ya jamii lilikuwa linalenga waajiriwa na kuacha nje waliojiajiri,takwimu zinaonyesha wastani watu 2000 kati ya zaidi ya watanzania milioni 50 wanaopata huduma ya hifadhi ya jamii na katika nchi yetu walioajiriwa ni wachache ukilinganisha na wale waliojiajiri"alisema.
Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawilo akisoma hotuba yake kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu katika ufunguzi wa semina ya mpango wa hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi kwa viongozi wa vikundi vya wajasiliamali na vyama vya ushirika Mkoani Kagera.
Baadhi ya viongozi 82 wa vikundi vya ujasiliamari na vyama vya ushirika Mkoani Kagera wakifuatilia mada mbalimbali zinazotolewa kuhusu mpango wa hifadhi ya jamii kwa sekta zisizo rasmi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad