KUBENEA AWATAKA VIONGOZI WA KISIASA KUFANYA KAZI, AKABIDHI MIRADI JIMBONI KWAKE - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

KUBENEA AWATAKA VIONGOZI WA KISIASA KUFANYA KAZI, AKABIDHI MIRADI JIMBONI KWAKE

Share This
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea ametoa mwito kwa viongozi mbalimbali nchini kuacha siasa na badala yake kufanyakazi kwa kwaajili ya maendeleo.

Kubenea ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipotembelea miradi ya maendeleo katika jimbo lake la Ubungo na kuikabidhi.

Miradi aliyoitembelea Kubenea ni ujenzi wa kibanda cha kupumzikia katika Zahanati ya Mavurunza iliyopo Kimara ambao umegharimu Sh. milioni 7.7, miradi wa ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Mabibo ambao umegharimu Sh. milioni 17,mradi wa kisima katika soko la Mabibo uliogharimu sh. milioni 12 pamoja na ujenzi wa ofisi za walimu katika Shule ya Msingi Kawawa.

Akizungumza baada ya kutembelea na kuikabidhi miradi hiyo, Kubenea amesema ni vyema kufanya kazi kwa kushirikiana na sio kuangalia chama."Mimi sifanyi mambo haya kwaajili ya siasa, ninafanya kwaajili ya maendeleo ya wananchi....ninajua hata siku nikiondoka itabaki historia kwamba Kubenea alifanya kitu fulani.

"Kwahiyo niwaombe viongozi wote, tusiangalie siasa eti huyu chama tawala, huyu Chadema...tufanye kazi pamoja katika kuleta maendeleo ya Taifa letu," amesema Kubenea.Amefafanua kuwa maendeleo yana safari ndefu hivyo maeneo ya jospitali na shule yanahitaji kuboreshwa.

Akizungumzia miradi hiyo Kubenea amesema fedha zake zimetoka katika mfuko wa jimbo ambapo ni sehemu ya fedha za bajeti ya mwaka 2017/18.Akitoa shukrani kwa ujenzi wa Kibanda cha mapumziko, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mavurunza amesema walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya msongamano wa wagonjwa ambao ulisababishwa na kutokuwa na sehemu ya kupumzika.

"Kwasasa tunafanya kazi kwa uhuru na usiri kati ya mgonjwa na daktari....tunakushukuru Mbunge wetu alia yemua kujitolea fedha hizi kutoka katika mfuko wako," amesema Dorothy.Aidha Dorothy amesema Zahanati hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo jengo la wazazi kuhitaji ukarabati, kutokuwa na uzio pamoja eneo hilo kuhitaji kusawazishwa ambapo Kubenea aliahidi atalisawazisha kwa kipindi kifupi.

Wakati huo huo Mkuu wa Shule ya Mabibo, Hussein Mabibo amesema fedha zilizotolewa ambazo ni sh. milioni 17 zimesaidia kujenga madarasa matano, kubadilisha vigae vilivyochakaa na kuweka mabati, kupanga rangi shule, kukarabati ofisi ya walimu pamoja na ofisi ya mwalimu Mkuu.

"Tunakuamini wewe Mbunge wetu ukisema hua unatekeleza, hivyo tunaomba utusaidie pia kukamilisha maktaba, ujenzi wa uzio wa shule kwaajili ya usalama wa wanafunzi pamoja na ukarabati wa madarasa tisa ambayo yako katika hali mbaya," amesema Dady.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Soko la Mabibo, Yusuph Kilema amesema kisima kilichojengwa katika soko hilo kimekamilika kwa asilimia 90 ambapo bado vitu vichache ili kianze kutumika rasmi.

Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na wakazi wa kata ya Mavurunza Kimara mara baada ya kukabidhi jengo la kupumzikia wagonjwa katika zahanati ya Mavulunza lililojengwa na fedha za mfuko wa jimbo
Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akiwa amembeba mmoja wa watoto waliofika kupata huduma katika Zahanati ya Mavurunza .
Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akisoma gharama za ujenzi wa Mnara wa kupandisha maji juu katika kisima kilichojengwa katika soko la Mabibo Garment kwa fedha za mfuko wa jimbo
Mhandisi wa maji wa Manispa ya Ubungo akitoa maelezo kwa Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea wakatia alipotembelea miradi iijengwa kwa fedha za mfuko wa jimbo.
Mwalimu wa shule ya Msingi Mkwawa Mabibo akimueleza Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea kiasi cha fedha zinazohitajika katika umaliziaji wa ofisi za walimu.
Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akiwa ameongozana na baadhi ya watendaji wa halmashauri na wafanyabishara wa soko la Mabibo
Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akisalimiana na wananchi na Makada Mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi.
Mmoja ya wakazi wa Mavurunza akitoa pongezi kwa Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea mara bada ya kutekeleza ahadi zake kwa wakazi wa eneo hilo 
wakazi wa Ubungo kata ya Mavurunza wakiwa wanasikiliza hotuba ya mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea 
Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mkwawa Mabibo-

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad