BALOZI WA KUWAIT AKABIDHI VIFAA TIBA KWA HOSPITALI KIGAMBONI - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

BALOZI WA KUWAIT AKABIDHI VIFAA TIBA KWA HOSPITALI KIGAMBONI

Share This
Ubalozi wa Kuwait umekabidhi zawadi ya vifaa tiba katika Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni ya Vijibweni vyenye thamani ya shilingi milioni 12 za kitanzania ikiwa ni utekelezaji wa mwanzo wa ushirikiano mzuri baina ya Kigamboni na Taifa la Kuwait. 

Akizungumza jana kwenye mapokezi ya vifaa tiba hivyo Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Mgandilwa ameshukuru kwa zawadi hizo alizozitoa Balozi wa kuwait ikiwa ni ahadi aliyoitoa alipotembelea Hospitalini hapo wiki mbili zilizopita. Mhe. Mgandilwa alisema kuwa matembezi ya Balozi wa Kuwait katika Hospitali ya vijibweni yalimfanya kubaini changamoto ya baadhi ya vifaa, hivyo kuahidi kurudi kabla ya mwezi wa ramadhani kuisha. 

Aliesma kuwa Kuwait na Tanzania ni marafiki na kuna kila sababu ya kuendelea kusapotiana na kudumisha urafiki uliopo huku akimuomba Balozi wa Kuwait kuendelea kusaidia baadhi ya vifaa ambavyo ameahidi atavileta kama vile vitanda vya kung'olea meno vitakavyosaidia kuboresha huduma za afya kwa ubora zaidi. 

"Naomba usiishie hapa kwa chochote utakaachona unaweza kusapoti kwenye sekta hizi tatu usisite kutusaidia na mimi kama Mkuu wa Wilaya naahidi kudumisha urafiki wetu" Alisema Mkuu wa Wilaya. Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem alisema zawadi alizozitoa ni mwanzo wa ushirikiano mzuri uliotokana na mapokezi mazuri aliyoyapata kipindi chote kutoka kwa Mkuu wa Wialaya ya Kigamboni pindi alipotembelea Wilayani kwake. 

Aliongeza kuwa Ubalozi wa Kuwait umetoa Vitanza 3 vya watoto, vitanda3 vya kujifungulia kinamama, mashine za oksijeni, mabeseni 8 ya watoto waliozaliwa , mashine ya kutolea uchafu pindi mtoto anapokunywa maji machafu wakati wa kujifungua na vifaa vingine ili kuboresha huduma za afya zinazotolea na Hopsitali ya Vijibweni. 

Balozi Jasem aliongeza kusema kuwa ataangalia namna atakavyoweza kusaidia kutoa mashine za moyo zilizoombwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni na kuahidi kuendeleza ushirikano uliopo na Kigamboni na Tanzania kwa ujumla. Aidha alisema kuwa Kuwait ina mpango unaojulikana kama Kuwait Blood Bank yenye lengo la kutunza damu salama hivyo atajitahidi kuhakikisha Kigamboni inakua miongoni mwa wanufaika wa mpango huo hususani Hospitali ya Vijibweni ambapo viataletwa vifaa vitakavyotumika kuhifadhia damu salama kwaajili ya kuokoa maisha ya Wananchi wa Tanzania. 

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe.Hoja Maabad alimshukuru Balozi wa Kuwait kwa zawadi alizozitoa na kumuomba kuendeleza urafiki na ushirikiano mzuri ulioanzishwa kwa manufaa ya wote. 

Imeandaliwa na: 
Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano 
Halmshauri ya Manispaa ya Kigamboni 
11/06/2018
 Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, leo tarehe 10/6/2018 amepokea ugeni wa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Najem.

Mapema akimkaribisha mgeni wake, DC Mgandilwa amemshukuru Balozi Najem kwa moyo wake wa upendo kwa  watanzania hususani wakazi wa Kigamboni. Ameeleza kuwa vifaa ambavyo vimetolewa ni vya zaidi ya Shilingi milioni kumi na moja na vinalenga kuondoa changamoto iliyokuwepo katika wodi za akina mama na watoto. 
Vifaa vilivyopokelewa ni pamoja na mashine za kusaidia wakati wa upasuaji, mashine za kusaidia kupumua, vifaa vya kupima moyo, vitanda vya watoto na beseni maalum kwa ajili ya akina mama wanaojifungua. 

DC Mgandilwa amesema kuwa nchi ya Kuwait ni miongoni mwa nchi ambazo ni marafiki wazuri wa Tanzania na kuwa Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kigamboni itaendeleza ushirikiano huo mwema. Kwa upande wake, Balozi Jasem Al Najem amewapongeza viongozi wa wilaya ya Kigamboni kwa ushirikiano mzuri ambao wamekuwa wakimpatia mara zote alipotembelea wilaya hiyo. 

Balozi Jasem ameeleza kuwa vifaa tiba alivyovikabidhi sio msaada bali ni zawadi kutoka kwa watu wa Kuwait kwenda kwa marafiki zao walioko Tanzania. 
Balozi Najem ameongeza kuwa huo ni mwanzo tu kwani baadhi ya vifaa tiba vingine vilivyoombwa na DC Mgandilwa atahakikisha vinapatikana na kuletwa ili kusaidia watu wa Kigamboni na watanzania kwa ujumla. 

Hafla ya kukabidhi vifaa tiba imefanyika katika hospitali ya  Vijibweni na baadae DC Mgandilwa alimkaribisha mgeni wake iftar iliyoandaliwa katika viwanja vya Msikiti wa Gaddafi uliopo Kigambobi.
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa akipokea sehemu ya vifaa tiba kutoka kwa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Najem.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad