WATEJA KUWASILIANA BILA KIKOMO NA SUPER HALO YA HALOTEL - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

WATEJA KUWASILIANA BILA KIKOMO NA SUPER HALO YA HALOTEL

Share This

Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii 

KAMPUNI ya mawasiliano ya simu ya Halotel, kwa mara ya kwanza imezindua kifurushi kisichokuwa na ukomo wa muda kitakacho wawezesha wateja wa mtandao huo kuwasiliana bila kikomo kupitia kifurushi kabambe cha Super Halo.

Wateja wa mtandao wa Halotel watakao jiunga na kifurushi hicho wataweza kupiga simu au kutumia intaneti hadi pale vifurushi vitakapokwisha muda wa matumizi.

Akizungumza katika uzinduzi uliofanyika katika Viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo Mhina Semwenda amesema kuwa, uzinduzi huo wa vifurushi vya Super Halo ni mapinduzi mengine makubwa katika sekta ya mawasiliano kwa kuondoa ukomo wa muda katika vifurushi vya muda wa maongezi na intaneti.

Amesema kama kampuni wamedhamiria kuwafurahisha wateja Kwa huduma kabambe za mawasiliano bila ya kuwa na wasiwasi wa kuisha kwa muda wa matumizi ya mawasiliano. Pia ameeleza kuwa mteja wa Halotel anaweza kujiunga kwa kuanzia shilingi 500 na kupata dakika 17 za kupiga Halotel bila kikomo cha muda na kwa shilingi 500 na kwa 500 hiyo hiyo mteja anaweza kujiunga na kupata MB 110 za intaneti za kutumia bila kikomo. 

Ameeleza lengo kubwa la kifurushi hicho ni kumwezesha mteja kuona thamani ya pesa yake na kuweza kufurahia mawasiliano ya kupiga simu na kutumia MB za intaneti bila kikomo.
 Baadhi Wateja wa Mtandao wa Halotel  wakiangalia vifaa mbalimbali vinavyo vinavyouzwa na kampuni ya simu ya  Halotel mara baada ya uzinduzi huo.
 Afisa Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala  akifafanua jambo mara baada ya uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Milimani City jijini Dar es  Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda akizungumza katika uzinduzi wa kifurushi kisichokuwa na ukomo kilichopewa jina na Super halo katika ukumbi wa Mlimani City  jijini Dar as Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad