WARSHA YA SIKU MOJA YAFANYIKA KUJADILI MPANGO KABAMBE WA MIAKA KUMI KUENDELEZA HIFADHI YA TAIFA YA MAHALE MKOANI KIGOMA. - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

WARSHA YA SIKU MOJA YAFANYIKA KUJADILI MPANGO KABAMBE WA MIAKA KUMI KUENDELEZA HIFADHI YA TAIFA YA MAHALE MKOANI KIGOMA.

Share This

Na Editha Karlo wa blog ya Jamii,Kigoma

WATANZANIA wametakiwa kujenga tabia ya kutembelea hifadhi za Taifa mbalimbali zilizopo nchini ili kuweza kujionea urithi na vivutio adimu vilivyopo kwenye hifadhi hizo.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga aliyasema hayo leo wakati warsha ya siku moja ya wadau mbalimbali wa Mkoani Kigoma wa Hifadhi ya milima ya mahale kilichokuwa kinajadili mpango kabambe wa miaka kumi wa kuendeleza hifadhi ya Taifa ya mahale.

Alisema katika Mkoa wa kigoma tumepata bahati ya kuwa na hifadhi mbili za Taifa ambazo ni hifadhi ya Taifa ya milima ya Mahale na Hifadhi ya Taifa ya gombe hivyo lazima juhudi za kutangaza hifadhi hizo ziongezeke.

"Tunajua Hifadhi ya mahale inachangamoto ya usafiri wa kufika kule kwani ili kufika inakulazimu kusafiri kwa njia ya maji kwa muda mrefu kutumia boti za kawaida,tunaomba mtuwekee speed boti, ila TANAPA mnafanya kazi kubwa ya kuhakikisha watalii wanaweze kufika Mahale kwa njia ya barabara"alisema Maganga

Maganga alisema kuwa mtu mmoja anapotembelea hifadhi ni sawa na watu kumi wametembelea kwani akitoka huko anakuwa balozi wa wengine.Mkuu huyo wa Mkoa alisema pia kupitia sekta ya utalii lazima iendane na kauli mbiu ya serekali ya sasa ya Tanzania ya viwanda."Hawa watalii kutoka nchi mbalimbali wanaokuja kutembea vivutio vyetu pia huwa wanaangali wapi pa kuwekeza tutumie fursa hizo za kuwashawishi waje kuwekeza nchini"alisema

Naye Ahmed Mbugi meneja wa ujirani mwema wa hifadhi ya milima ya mahale kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa shirika la hifadhi la Taifa(TANAPA)Allan Kijazi amesema kuwa ili mpango huo uweze kufanikiwa wamekusanya maoni mbalimbali ya wadau kuanzia ngazi ya kijiji hadi Mkoa na leo maoni hayo wanayawasilisha kwa wadau mbalimbali kupitia warsha hiyo.

Mbugi alisema kuwa wao kama shirika wanajitahidi mahitaji yote muhimu yanapatikana kwa wageni wanaoenda kutembelea hifadhi.Alisema Hifadhi ya milima ya mahale inachangamoto ya usafiri ambapo miundombinu ya barabara ya kwenda huko haikuwa rafiki hapo awali lakini sasa hivi toka barabara itengenezwe watalii wameongezeka kwenda mahale.

Alisema kupitia mpango huo kabambe wa kuendeleza hifadhi ya milima ya mahale ambao umewashirikisha wadau wa ngazi zote baada ya miaka kumi hifadhi ya milima ya mahale ili kukabiliana na changamoto zinazoikumba hifadhi hiyo.
 Picha ya pamoja baina ya wadau mbalimbali wa utalii wa Mkoa wa Kigoma na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia jenerali mstaafu Emanuel Maganga muda mfupi baada ya kuzindua warsha ya kujadili mpango kabambe wa miaka 10 wa kuendeleza hifadhi ya milima ya mahale
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa utalii wa Mkoa wa kigoma inayojadili mpango kabambe wa miaka 10 ya  kuendekeza hifadhi ya Milima ya Mahale
 Meneja wa ujirani wa hifadhi ya milima ya Mahale, Ahmed Mbugi akielezea hifadhi ya milima ya mahale kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa TANAPA Allan Kijazi kwenye kikao cha wadau wa utalii wa kuendeleza hifadhi ya Mahale
 Wadau wa utalii wa Mkoa wa Kigoma wakiwa katika warsha ya siku moja ya kupitisha mipango kabambe ya miaka 10 ya kuendeleza hifadhi ya milima ya mahale

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad