TTCL YAENDELEA KUTOA LINE BURE MTWARA - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

TTCL YAENDELEA KUTOA LINE BURE MTWARA

Share This

JOSEPH MPANGALA , MTWARA

Kampuni ya Mtandao wa sim TTCL Cooperation Imeendelea Kutoa na Kusajili line za sim Bure ili kuwawezesha wateja wake wapya kuweza kuwasilina kwa bei nafuu pamoja na kujiunga na vifurushi vya Internet.

Akiongea katika Kiwanja Cha mashujaa kilichopo mkoa wa mtwara katika Promosheni ya NYAKA NDINGA inayoendeshwa na kituo cha Radio cha EFM/TVE Meneja wa Mkoa Mhandisi Rumishael f. Temba anasema TTCL imeanzisha Bando kwa ajili ya internet ambayo wateja wengi wamekuwa wakiyapenda na Kuyatumia kwa wingi.

“Katika Upande wa mabando kwa TTCL ambayo wateja wake wanayapenda zaidi ni Boom Pack kwa ajili ya wanachuo,Serereka Bando la Kijanja ambalo kila mwananchii anaweza kulipata kwa bei nafuu pamoja na bando la Toboa”

Aidha TTCL imetambulisha Huduma ya T-pesa kwa mtandao ambapo unaweza kutumia kulipia Huduma ya LUKU bila ya kuwa na gharama za ziada.
 Meneja wa Mkoa TTCL Cooperation Mhandisi Rumishael f.Temba akiongea na Wananchii kuhusina na Huduma Zinazotolewa na kampuni Hiyo wananchii waliokuja katika Promosheni ya Nyaka Ndinga Inayoendesha na EFM na TVE.
 Baadhi ya wateja wakiwa wamezunguka Banda la TTCL kwa ajili ya kupata Huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni hiyo.
 Meneja wa Mkoa TTCL Cooperation Mhandisi Rumishael f.Temba akitoa zawadi kwa Washiriki Kumi watakaokwenda Dar es Salaam kwa ajili ya shindano kubwa la promosheni ya Nyaka Ndinga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad