728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, May 14, 2018

  Tanzania Health Summit yachangia shilingi milioni moja kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu ya upasuaji wa moyo kwa mtoto mmoja

   Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wa    Tanzania Health Summit wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa mfano wa  hundi ya shilingi milioni moja fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu ya upasuaji wa moyo kwa mtoto Mbaruku Kabwe aliyelazwa JKCI  kwa ajili ya matibabu. Kushoto ni mama wa mtoto Asha Omary mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
  Rais wa  Tanzania Health Summit Dkt. Omary Chillo akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi hundi ya shilingi milioni moja kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu ya upasuaji wa moyo kwa mtoto Mbaruku Kabwe aliyelazwa katika Taasisi hiyo kwa ajili ya matibabu. Kila mwaka  Tanzania Health Summit wanaandaa mashindano ya Heart Marathon lengo likiwa  ni kusaidia watoto wanaosumbuliwa na  magonjwa yasiyoambukiza ukiwemo ugonjwa wa moyo.Picha na JKCI
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Tanzania Health Summit yachangia shilingi milioni moja kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu ya upasuaji wa moyo kwa mtoto mmoja Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top