728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, May 6, 2018

  SIR ALEX FERGUSON AFANYIWA UPASUAJI KATIKA UBONGO WAKE, AWEKWA CHINI YA UANGALIZI MAALUM

  Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

  Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Manchester United, Sir Alex Ferguson imebainika amefanyiwa Upasuaji katika Ubongo wake baada ya hapo awali kuripotiwa kuumwa ghafla.


  Manchester United kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter imetoa taarifa ya kuumwa kwa Sir Ferguson kwa kusema kuwa "Tayari ameingia kufanyiwa upasuaji wa Ubongo wake na zoezi linaendelea vizuri lakini anahitaji kuwa katika Uangalizi maalum kwa msaada ili arudi katika hali yake ya kawaida".

  Kabla yakuumwa, Sir Alex Ferguson hapo nyuma alinekana katika mchezo kati ya Man United dhidi ya Arsenal, Old Trafford wakati wakumuaga Kocha wa Washika Mitutu wa London (Gunners), Arsene Wenger anayeondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.


  Sir Alex Furguson alishinda Mataji 13 ya Ligi Kuu Soka nchini Uingereza katika kipindi cha miaka 26 alipokuwa akiifundisha Manchester United kabla yakustaafu mwaka 2013.

  Chanzo: Goal. com
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SIR ALEX FERGUSON AFANYIWA UPASUAJI KATIKA UBONGO WAKE, AWEKWA CHINI YA UANGALIZI MAALUM Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top