LULU KUFANYISHWA KAZI ZISIZO NA MALIPO KWA MANUFAA YA UMMA - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

LULU KUFANYISHWA KAZI ZISIZO NA MALIPO KWA MANUFAA YA UMMA

Share This


Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imesema mfungwa Na. 1086/2017 Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu atatumia kifungo chake nje ya gereza kwa kufanya shughuli au kazi siziso na malipo kwa manufaa ya jamii.

Lulu ambaye ameachiliwa Mei 12 mwaka huu (Jumamosi)anakwenda kutumia kifungo chake nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania na sababu za kutumia kifungo hicho nje kumetokana na kukidhi vigezo vya kisheria na kuonesha tabia njema akiwa gerezani.

Taarifa ya Jeshi la Magereza iliyotolewa leo jijinni Dar es Salaam imeeleza Aprili  26 mwaka huu katika kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya ibara ya 45(1) ya Katiba alitoa msamaha wa 1/4 ya adhabu kwa wafungwa wote waliokuwa na sifa za kunufaika na msamaha huo.

"Kutokana na msamaha huo Lulu alinufaika na msamaha huo

na Mei 12 mwaka huu ametolewa gerezani na kwenda kutumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu Tanzania,"imesema taarifa ya Jeshi la Magereza.

Hata hivyo licha ya sheria kuelezea kuwa Lulu anatakiwa kufanya shughuli za kijamii bila malipo yeyote haijaweka wazi ni kazi gani ambayo atakwenda kuifanya baada ya kuwa nje.

Lulu kabla kabla ya msamaha huo alikuwa akitumikia kifungo cha miaka miwili jela katika Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam baada ya kupokelewa gerezani hapo Novemba 13 mwaka 2017.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad