WAHAMASISHWA KULIPA YA KODI YA ARDHI MTWARA - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

WAHAMASISHWA KULIPA YA KODI YA ARDHI MTWARA

Share This
NA   JOSEPH MPANGALA- MTWARA.

Wamiliki wa Viwanja na mashamba waliopo kanda ya kusini,Mikoa ya Lindi Ruvuma na Mtwara wametakiwa kulipa Kodi ya Ardhi pamoja na malimbikizo ya Yamadeni kwa mwaka wa fedha 20017/2018ili kuepuka usumbufu wakupelekwa mahakamani,Kunadiwa malizao au kufutiwa miliki ya ardhi zao. 

Kodi hii inatakiwa kulipwa kila tarehe 1Julai hadi mwezi disemba kila mwaka na ifikapo januari mosi ya kila mwaka kodi hii hulipwa pamoja na adhabu ambayo ni asilimi1 kwa kila mwezi wa kodi husika. 

Akiongea na waandishi wa habari ofisin za kanda ya kusini mkoani Mtwara Kamishna Msaidizi wa ardhi Kanda ya Kusini Gasper Luanda amesema wananchii woote wanaomiliki Viwanja na Mashamba kwenda ofisi za Halmashauri za Wilaya,Miji,manispaa pamoja na Ofisi za kanda kwa ajili ya kupata Makadirio ya Ankara za malipo. 

“Tangazo hili linamuhusu mtu yeyote mwenye kiwanja na aliyemilikishwa lakini hata Yule aliyemilikishwa na amejenga kwa hiyo kama una jengo lako kwenye kiwanja ulichopewa inamana utalipa kodi mbili,Utalipa kodi ya ardhi kwenye wizara ya ardhi lakini kwa kupitia mawakala wetu ambao ni Halmashauri lakini sasa hivi tunamawakala kupitia banki za NMB na CRDB lakini ya kodi ya pango la ardhi unakwenda kulipiwa TRA kwa hiyo wananchii wasichanganye hizi kodi mbili kila moja inasimamiwa na Sheria zake. 

Aidha Luanda ameongeza kuwa muitikio wa ulipaji kodi ya majengo,Vianja na mashamba katika kanda ya kusini umekuwa mkubwa kutokana na Makadirio waliopewa ya ukusanyaji kuendelea kuongezeka kila mwezi. 

“Muitikio ni Mzuri kama mnavyojua makusanyo ya kodi yanakwenda na malengo sisi kama kanda Tulipewa jukumu la kukusanya Kodi ya Billion7.86 kanda kwa maana mikoa yote ya Mtwara Lindi na Ruvuma sasa watu wamelipa na Tunakaribia sasa Billion saba na Kitu lakini sasa kuna pengo la million mia sita/mia saba hivi halijakusanywa ndio maana tupo hapa kuwahimiza wale wachache ambao wamebaki basi nao watimize wajibu wao kwa sasabu kulipa kodi ni Lazima sio Hiari” 

Kwa sasa Miggogoro katika Mkoa ya kanda ya kusini imeonekana kupingua kutokana na Kuweka Dawati la Migogo ambalo linasikiliza Migogoro ambapo kwa sasa wanaokuja kulalamika wamepunua kwa kiasi kikubwa. 
Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kusini Gasper .V.Luanda akongea na waandishi wa habari kuhusiana na Uahamisishaji wa Ulipaji wa kodi kwa wamiliki wa Viwanja na mashamba katika kanda ya Kusini Mikoa ya Lindi,Ruvuma pamoja na Mtwara.
Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kusini Gasper .V.Luanda wakifurahi jambo na Afisa Mipango miji Manispaa ya Mtwara Mikindani Mkono Werema wakati wa kipindi cha Maswali na majibu na waandishi wa habari juu ya kodi kwa wamiliki wa Viawanja na mashamba Mkoani Mtwara

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad