IGP SIRRO AWAPA SOMO WASTAAFU POLISI. - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

IGP SIRRO AWAPA SOMO WASTAAFU POLISI.

Share This
Na. Jeshi la Polisi. 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewaasa Makamishna wastaafu wa Polisi kuendelea kukabiliana na uhalifu wawapo uraiani baada ya kustaafu utumishi wa Polisi kwa kuwa mapambano ya uhalifu hayana mipaka. 

IGP Sirro aliyasema hayo jana wakati wa hafla maalum ya kuwaaga waliokuwa Makamishna wa Polisi, Glodwing Mtweve na Elice Mapunda katika viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, hafla ambayo ilihudhuriwa na maafisa wakuu wa Polisi, Askari na familia za wastaafu hao. 

“Mmefanya kazi kubwa sana wakati mlipokuwa nasi na uzoefu wenu tutaendelea kuuhitaji na kuutumia lakini sasa mnaporudi uraiani haina mana kuwa hamruhusiwi kuendeleza mapambano ya uhalifu la hasha hii ni fursa sasa ya kuwasaidia wananchi kupata mbinu ili kwa pamoja mshirikiane na Jeshi la Polisi kuukabili uhalifu kwa kuwa mtakuwa karibu na jamii zaidi” Alisema IGP Sirro. 

Kwa upande wake Kamishna Mstaafu Clodwin Mtweve amewataka Maofisa na Askari Polisi kuendelea kufanya kazi zao kwa kujituma na weledi ili kuhakikisha kuwa uhalifu unaendelea kupungua kwa kuwa uhalifu sasa unafanywa kisayansi. 

Mtweve amesema wanaoendelea kulitumikia Jeshi la Polisi hawana budi kuyafuata yale mazuri yote waliyofanya na yale mabaya kuyaacha ili nao waweze kumaliza salama utumishi wao salama na kuagwa kama ilivyokuwa kwao. 

Naye Kamishna mstaafu Elice Mapunda ambaye alikuwa Mwanamke wa kwanza kufikia cheo cha kamishna wa Polisi tangu kupata uhuru aliwataka askari wa kike nchini kujituma ili kupata mafanikio kama ilivyo kwa wanaume kwa kuwa kupata vyeo ndani ya jeshi hilo hakuangalii jinsia bali ni utendaji wa kazi. 

Amesema askari wa kike hana tofauti na wa kiume kwa kuwa mafunzo wanayopitia ni ya aina moja hivyo wakijituma zaidi na kufanya kazi zao kwa ufanisi wataonekana na kupewa madaraka kwa mujibu wa taratibu na kanuni za Jeshi hilo. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad