Halmashauri Wilaya ya Longido yapewa siku 7 kuhakikisha imejibu hoja zote zilizotolewa na mkaguzi wa nje (CAG) - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

Halmashauri Wilaya ya Longido yapewa siku 7 kuhakikisha imejibu hoja zote zilizotolewa na mkaguzi wa nje (CAG)

Share This
Halmashauri ya Wilaya ya Longido imepewa siku 7 kuhakikisha imejibu hoja zote zilizotolewa na mkaguzi wa nje (CAG) kwa mwaka fedha kuanzia 2015 hadi 2017.

Akitoa agizo hilo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amesema halmashauri kupata hati ya mashaka kwa hoja zinazojibika na zinazojirudia kila mwaka ni uzembe wa baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo.

“Watumishi bado wapo wachache wanaofanya kazi kwa mazoea bila ya kufuata sheria na taratibu za kiutumishi”.Ameuwagiza uongozi wa halmashauri ya Longido kutoa barua za onyo kwa watumishi wote waliotajwa kwenye taarifa ya mkaguzi wa nje ili iwe fundisho kwa watumishi wote umma.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega,amesema ifike wakati sasa viongozi kutoonea huruma mtumishi yoyote anaebainika ana makosa, kwani hoja nyingi katika halmashuri hiyo zimekuwa zikijirudiarudia kila mwaka.Amesema hatua madhubuti ni lazima sasa zichukuliwe ili kudhibiti tabia hii ya mazoea ya hoja kujirudiarudia kila mala.

Akisisitiza zaidi mkuu wa wilaya ya Longido Daniel Chongolo amesema kazi ya viongozi ni kusimamia sheria na taratibu za kazi,hivyo ataendelea kusimamia sheria za utumishi wa umma katika halmshauri yake kwani mpaka sasa hali imeanza kubadilika kwa watumishi kuwa na nidhani.

Aidha, amesema halmshauri ipo tayari kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na mkuu wa mkoa na kuhakikisha halmashauri yake haitapata tena hati ya mashaka kwa miaka inayokuja.Gambo yupo katika ziara ya siku 3 wilayani Longido ambapo atatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanywa katika wilaya hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Longido alipokuwa akuzungumzia hoja za CAG.
Mkuu wa Wilaya ya Longido Daniel Chongolo akimchukuru Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo baada ya kutoa maelekezo ya namna ya kujibu hoja za CAG.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo, akisoma baadhi ya hoja zilizotolewa na mkaguzi wa nje (CAG) katika kikao chake na watumishi wa halmashauri ya Longido.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad