DC SHINYANGA AFUNGUA WARSHA YA MASUALA YA JINSIA KWA WALIMU ILIYOANDALIWA NA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

DC SHINYANGA AFUNGUA WARSHA YA MASUALA YA JINSIA KWA WALIMU ILIYOANDALIWA NA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA

Share This
Warsha hiyo iliyoandaliwa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania tawi la Shinyanga kwa ufadhili wa benki ya CRDB tawi la Shinyanga imefanyika leo Jumatatu Mei 14,2018 katika chuo hicho mjini Shinyanga kwa kukutanisha walimu 100.Warsha hiyo ni sehemu ya Mpango Maalumu uliobuniwa na Chuo hicho kwa ajili ya kujenga uwezo watumishi wa umma hasa walimu juu ya masuala ya jinsia.

Akifungua warsha hiyo,Matiro alisema mbinu stahiki za kupambana na ukatili wa kijinsia zitafanikiwa endapo dhana,aina,matokeo na sababu za ukatili zitaeleweka kuanzia ngazi ya msingi hususani shuleni ambapo watoto wanatumia muda mwingi wa maisha yao.“Niwapongeze sana kwa kuanzisha mpango huu wa kuwafikia walimu,warsha hii ni nyeti sana na huenda kuna walimu ambao walishawahi kushuhudia ama kutenda vitendo vya kibaguzi kwa watoto kwa kujua ama kutojua,kwa hali hii vitendo hivyo vina athari kubwa katika maendeleo ya kitaaluma kwa watoto”,alisema Matiro.

Aidha alisema ni jukumu la walimu na shule kuweka kanuni na taratibu ambazo zitatoa ulinzi na kusaidia jamii nzima ya shule kuishi kwa amani na kuzingatia usawa.“Niwaombe msiishie kwa walimu pekee kutoa elimu hii,bali wafikieni pia watumishi wote wa umma kwani nao kwa sehemu yao wana mchango mkubwa katika ujenzi wa jamii inayothamini usawa wa kijinsia”,aliongeza.

Mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza wakati wa warsha hiyo.Kushoto ni Mratibu wa Masuala ya Jinsia katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania tawi la Shinyanga,Getrude Pastory Massawe ambaye pia Afisa Masoko wa chuo hicho.Kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,Kituo cha Shinyanga, Paschal Mheluka.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza katika warsha hiyo na kueleza kuwa kukosekana kwa usawa baina ya wasichana na na wavulana shuleni na katika jamii ni chanzo kikuu cha ukatili kitu kinachofanya ukatili kuwa suala la kijinsia.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,Kituo cha Shinyanga, Paschal Mheluka akizungumza wakati wa warsha hiyo iliyokutanisha walimu 100 kutoka shule za msingi na sekondari zilizopo katika manispaa ya Shinyanga.
Mratibu wa Masuala ya Jinsia katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania tawi la Shinyanga,Getrude Pastory Massawe ambaye pia Afisa Masoko wa chuo hicho akizungumza wakati wa warsha hiyo ambapo alisema wameamua kuanzisha mpango wa kutoa elimu ya masuala ya jinsia kwa walimu ili kuhakikisha walimu hao wanatoa elimu kwa wanafunzi wao kumaliza vitendo vya ukatili katika jamii.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad