BARAZA LA MITIHANI LATANGAZA KUANZA MITIHANI KIDATO CHA SITA,UALIMU - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

BARAZA LA MITIHANI LATANGAZA KUANZA MITIHANI KIDATO CHA SITA,UALIMU

Share This

*Watakaofanya udanganyifu wa aina yoyote kukiona cha moto

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BARAZA la Mitihani la Tanzania(Necta) limetoa onyo kali kwa wamiliki wa shule,walimu na wananchi kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu wa mitihani ya Kidato cha Sita na Kozi za ualimu inayoanza kesho Mei 7 hadi Mei 25 mwaka huu.

Kwa mujibu wa baraza hilo  ni kwamba jumla ya watahiniwa 87,643 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita ambapo kati yao watahiniwa wa shule ni 77,222 na watahiniwa wa kujitegemea ni 10,421.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa Necta Dk.Charles Msonde ametangaza kuanza kwa mitihani hiyo ambapo ameonya watu kutojihusisha na udanganyifu wa aina yoyote.Akisisitiza Dk.Msonde amesema baraza la mitihani halitasita kumchukulia hatua yeyote atakayejihusisha kufanya udanganyifu katika mihitani kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma na sheria za nchi.

Amefafanua ikiwa panoja na kuwafutia matokeo yote watahiniwa watakaobainika kujihusisha na vitendo vya udanganyifu."Wadadau wore wanaombwa kutoa taarifa katika vyombo husika kila wanapobaini uwepo wa mtu au kikundi cha watu kujihusisha na udanganyifu wa mitihani wa aina yoyote ile," amesema Dk.Msonde.Pia amesema baraza linatoa mwito kwa jamii kutoa ushirikiano katika kuhakikisha mitihani hiyo inafanyika kwa amani na utulivu .

"Wananchi wanaombwa kuheshimu eneo la mitihani na kuhakikisha asiyehusika  haingii maeneo ya shule,"amesema Dk.Msonde.Ameongeza wamiliki wa shule na vyuo wanatakiwa kutambua shule na vituo vya maalum vya mitihani  na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingiliwa majukumu ya usimamizi wa mitihani kwa kipindi chote hicho.

" Baraza halitosita kukifuta kituo chochote cha mtihani endapo litajiridhisha kuwa uwepo wake ubahatarisha usalama wa mitihani ya Taifa,"amesema Dk.Msonde.Ametumia nafasi hiyo kutoa mwito kwa kamati za mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha taratibu zote za uendeshaji mitihani ya Taiga zinazingatiwa ipasavyo.

Kwa upande wa wawatahiniwa ,amesema baraza linaamini walimu wamewaandaa vizuri katika kipindi chote cha elimu ya sekondari na kozi za mafunzo ya ualimu.Hivyo matarajio yao watahiniwa watafanya mitihani yao kwa kuzingatia kanuni za mitihani ili matokeo yaoneshwe uwezo wao halisi kulingana na maarifa na ujuzi walioupata kipindi cha mafunzo yao.
 Katibu Mtendaji wa Necta Dk.Charles Msonde akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo alipokuwa akitangaza kuanza kwa mitihani hiyo ambapo ameonya watu kutojihusisha na udanganyifu wa aina yoyote.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad