SERIKALI INAFANYA TATHIMIN YA FIDIA ARIDHI NA MAENDELEZO YAKE MPAKA WA TANZANIA, KENYA - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

SERIKALI INAFANYA TATHIMIN YA FIDIA ARIDHI NA MAENDELEZO YAKE MPAKA WA TANZANIA, KENYA

Share This


Na Rehema Isango, Tarime, Mara

SERIKALI inafanya tathmini kuhusu fidia ya ardhi na maendelezo yake katika eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya iwapo kutakuwa na utwaaji ardhi wakati wa zoezi la kuimarisha mpaka linaloendelea mkoani Mara.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Doroth Mwanyika alisema hayo wakati alipokagua kazi ya uimarishaji mpaka katika eneo la upande wa pwani ya Ziwa Victoria mkoani Mara katika kijiji cha Kirongwe kata ya Bukura Wilayani Rorya hadi eneo la Sirari mkoani Tarime.

Amefafanua Serikali inafanya tahmini hiyo kwa lengo la kuona wananchi waliopo katika eneo huru (buffer zone) iwapo watatakiwa kupisha eneo hilo, itumike njia bora ya kujadiliana nao au namna mbadala ya kuwasaidia wananchi hao.

“Kwanza wananchi walioendeleza maeneo ya mipakani walipewa elimu wakati wa mchakati wa uhamasishaji lililofanywa na wataalam wetu kabla ya kuanza kwa kazi ya uimarishaji mpaka." Wengine wameelewa na kuchukua hatua ya kupisha wakati kazi ya uimarishaji mpaka inaendelea,” amesema Mwanyika.

Aidha Serikali imebainisha kuwa itahakikisha inatatua changamoto hizo zilizojitokeza katika zoezi hilo kwa njia ya amani na kwa kuzingatia haki. Mapema Machi mwaka huu, Serikali za pande zote mbili Tanzania na Kenya zilikubaliana kuanza kazi ya uimarishaji wa mpaka wa Kimataifa katika urefu wa kilomita 238 za nchi kavu kutoka ziwa Victoria mkoani Mara hadi Ziwa Natroni mkoani Arusha.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Doroth Mwanyika ( wa tatu kutoka kushoto  aliyeinama) akigusa moja ya alama mpya zinazoongezwa kila baada ya urefu wa mita mia moja kwenye mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Kenya. Bibi Mwanyika na Makatibu Wakuu wengine wanne walikagua mpaka huo wakati wa kazi ya uimarishaji iliyoanza Machi mwaka huu. Picha zote na Rehema Isango WANMM

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad