WAZIRI MKUCHIKA AKUTANA NA UJUMBE WA DfID - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

WAZIRI MKUCHIKA AKUTANA NA UJUMBE WA DfID

Share This
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) akiwa katika kikao na ujumbe kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DfID) nchini Tanzania, (hawapo pichani) ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) akiwa katika kikao na ujumbe kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DfID) nchini Tanzania, ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. 
Kiongozi wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DfID) nchini Tanzania, Bi. Beth Arthy akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) hayupo pichani wakati wa kikao leo jijini Dar es Salaam.
Kiongozi wa ujumbe kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DfID) nchini Tanzania, Bw. Nicholas Leader akiwa katika kikao na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) hayupo pichani, ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.DfID MDAU WA MAENDELO WA SERIKALI YA TANZANIA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) ameishukuru Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DfID) kwa kuwa moja kati ya wadau wa maendeleo nchini.

Mhe. Mkuchika amesema hayo leo katika kikao na ujumbe kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DfID) kilichofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam.Ninapenda kuishukuru DfID pamoja na Serikali ya Uingereza kwa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania ili kuleta maendeleo kwa Watanzania wote.

Mhe. Mkuchika amesema DfID kama moja ya washirika wa maendeleo wamechangia kwa kiasi kikubwa jitihada za serikali za kupambana na rushwa, na moja ya matokeo yake ni kuongeza uwajibikaji katika utoaji huduma kwa wananchi na kuondosha rushwa kupungua.

Mhe. Mkuchika ameuhakikishia ujumbe wa DfID kuwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iko tayari muda wowote kushirikiana na DfID katika kuleta maendeleo.Kiongozi wa DfID nchini, Bi. Beth Arthy ameahidi kuendeleza ushirikiano katika utekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad