VIONGOZI WA MKOA WA RUKWA WAAGIZWA KUTOKOMEZA UDUMAVU UNAOSABABISHWA NA LISHE DUNI. - JIACHIE

JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad

VIONGOZI WA MKOA WA RUKWA WAAGIZWA KUTOKOMEZA UDUMAVU UNAOSABABISHWA NA LISHE DUNI.

Share This

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akijiridhisha na uwepo wa Dawa katika stoo ya Dawa katika kituo cha Afya cha Mazwi.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akiongoza msafala wa ukaguzi wa jingo jipya  katika kituo cha Mazwi Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akikagua Dawa katika stoo ya Dawa katika Kituo cha Afya Mazwi, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mkoa wa Rukwa wilaya ya Sumbawanga, pembeni yake ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Boniface Kasululu.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akiwa ndani ya jengo jipya la wodi ya kina mama wajawazito, katika ziara yake ya kukagua huduma zinazotolewa katika kituo hicho.
 

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akipitia ramani ya jengo jipya la mama na mtoto linaloendelea kujengwa katika hatua ya kuboresha huduma katika kituo cha Afya cha Mazwi.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akiteta jambo na viongozi mbali mbali katika moja ya jengo jipya linalojengwa katika kuboresha kituo cha Afya cha Mazwi.
 
 
Na WAMJWW. RUKWA-SUMBAWANGA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Rukwa kuhakikisha wanapambana na kutokomeza udumavu kwa watoto unaosababishwa na ukosefu wa Lishe bora.

Ameyasema hayo akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua shughuli za utoaji huduma za Afya, na uhamasishaji wa vikundi vidogo vidogo vya wanaweke vya ujasiriamali katika Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.

”Mkoa wa Rukwa haupaswi kuwa na utapiamlo hata kidogo, asilimia 60 ya udumavu ndani ya Rukwa ni kiasi kikubwa sana, katika mkoa ambao una chakula na ardhi yenye rutuba nzuri ni jambo la kushangaza kuona tatizo hili”, Alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile aliendelea kwa kusema kuwa, Siku 100 za mwanzo tangia mtoto anazaliwa ni muhimu na nyeti sana katika kuhakikisha anapata maziwa ndani ya miezi sita, na anapoanza kula ale vyakula vyenye lishe ya kutosha ili ubongo wake ukue vizuri.

Aidha, Dkt. Ndugulile ametoa maelekezo kwa sekretarieti ya Mkoa na viongozi wa kisiasa kushirikiana kwa pamoja katika kutoa elimu ya kutosha kwenye kila mikusanyiko watakayofanya kuhusiana na masuala ya Lishe bora ili kutokomeza janga hili linalosumbua idadi kubwa ya watoto katika Mkoa huu.

Kwa upande wake Mbunge wa Sumbawanga Mh. Aishi Hilaly amemshukuru Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kwa kuwakumbuka katika mgao wa fedha za kuboresha Vituo vya Afya cha Mazwi, pia hakusita kupaza sauti juu ya ombi la gari la kubebea wagonjwa litakalosaidia kupunguza hadha kubwa wanayokumbana nayo inayotokana na kukosekana kwa gari hilo.

Nae Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Boniface Kasululu Mkoa unaendelea kupambana na magonjwa ya mlipuko hasa ugonjwa wa kipindupindu kwa kutoa elimu ya Afya na Usafi wa mazingira kwa wananchi, ili kuhakikisha magonjwa haya yanakuwa historia katika mkoa wa Rukwa.

Aidha, Dkt. Kasululu alimuomba Dkt. Faustine kupunguza hadha ya upungufu wa madaktari bingwa na mabingwa wa fani nyingine, Dkt. Kasululu alisema kuwa hadi kufikia Desemba 2017 Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa inajumla ya madaktari bingwa 5 ambao ni sawa na asilimia 21 kati ya madaktari 24 wanaohitajika.
 
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad