728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, August 3, 2017

  WASANII WA BONGO FLEVA WAASWA KUZINGATIA MATUMIZI YA LUGHA.

  Wasanii wa Bongo Freva  hapa nchini wameaswa kuzingatia matumizi ya Lugha pamoja na mavazi  ili kuepusha fungia fungia ya kazi zao za sanaa.

  Hayo yamesemwa leo wakati wa mkutano wa  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe na wasanii wa nyimbo za bongo Freva pamoja na wadau mbalimbali na sanaa hapa nchini jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wasanii wa nyimbo za Bongo Freva hapa nchini kuhusu maswala mbalimbali yanayowahusu wasanii hao, pia wameshauliwa kujiunga kusajili kazi zao pamoja na kulipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kupata miongozo mbali mbali COSOTA pamoja na BASATA.
   Baadhi ya wasanii wa Nyimbo za Bongo Freva  hapanchini kutoka kulia ni Wastara Thomasi, msanii wa Bongo Fleva, Khadija Shaban (Keisha) na Witnes Mwajaga wakiwa katika Mkutano wa wasanii wa Bongo freva na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe jijini Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea saa ya ukutani ikiwa ni Rambirambi kutoka kwa wasanii wa Mziki wa Bongo Freva  kama pole kufiwa na Mkewe.
                     Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii. 


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WASANII WA BONGO FLEVA WAASWA KUZINGATIA MATUMIZI YA LUGHA. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top