728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, August 9, 2017

  WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU YAJA NA MASHINE YA KISASA YA KUKATIA MAGOGO

  Na Chalila Kibuda, Lindi.

  WANANCHI wa Mkoa wa Lindi wamehamasishwa kutumia mashine ya kukatia mbao  (WOODMISER ) ili waweze kurahisha kazi pamoja na muda kwa kutumia mashine za zamani.

  Akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya Nanenane mkoani Lindi, Meneja wa Mawasiliano wa Wakala wa Huduma za  Misitu nchini, Grlory Mziray amesema kuwa mashine hiyo ni nzuri kwa matumizi ya kukatika magogo  na kuzalisha mbao nyingi kutokana na mabaki yake kuwa madogo ukilinganisha na mashine zingine.

  Amesema kuwa huduma zinazosimamiwa na wakala za misitu unahamasisha wananchi kuwa uhifadhi wa misitu ni jukumu la kila mtanzania katika kuitunza na kuisimamia ili kuhakikisha faida zake zinatumika kwa kwa kizazi kilichopo na cha baadae.

  “Misitu ni hewa tunayovuta misitu ni maji pamoja na rutuba ya ardhi yetu inategemea misitu , misitu hiyo hiyo inategemea kuitunza”amesema Glory

  Amesema nyuki ni bidhaa isiyohitaji kulindwa lakini inatoa bidhaa tano zinazoweza kusaidia kutunza misitu hiyo wananchi wanahitaji kupatiwa elimu ya ufugaji nyuki kutoka kwa wakala wa huduma za misitu ambazo ziko katika kila wilaya ili waweze kutumia fursa zilizopo zitokazo na asali katika kwenda katika uchumi wa viwanda wa serikali ya awamu ya tano kutokana na kuwepo kwa masoko makubwa ya asali.
   Wananchi wakiangalia mashine ya kukatia magogo katika maonesho ya Nanenane yaliyofikia mwisho jana katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
   Mhifadhi wa Mambo ya Kale, Paul Nyelu akiwapa maelezo wananchi  na wanafunzi waliotembelea banda Wizara ya Maliasili na Utalii juu ya vipindi vya historia ambayo nchi imepita  katika katika maonesho ya Nanenane yaliyofikia mwisho jana katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
   Afisa wa Misitu, Ahazi Shayo akitoa maelezo juu ya huduma za wakala wa misitu inavyofanya kazi katika maonesho ya Nanenane yaliyofikia mwisho jana katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
  Wananchi wakiwa  katika sherehe za Nanenane katika maonesho yaliyofikia mwisho jana katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU YAJA NA MASHINE YA KISASA YA KUKATIA MAGOGO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top