728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, August 11, 2017

  Mshindi wa Milioni 20 za Biko Kimara Suka akabidhiwa fedha zake

  MSHINDI wa Shilingi Milioni 20 za Biko kutoka kwenye Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, Anthony Chitanda, amekabidhiwa fedha zake mapema jana katika benki ya NMB, Tawi la Bank House, Posta, jijini Dar es Salam, sambamba na kupewa ushauri wa kifedha.

  Chitanda aliibuka kidedea katika droo ya 30 ya Biko iliyochezeshwa juzi Jumatano na kuvuna Sh Milioni 20 zinazotolewa na waendeshaji hao wa Biko, mchezo wa kubahatisha unaoendelea kutingisha katika wilaya na mikoa mbalimbali ya Tanzania.


  Akizungumza katika Makabidhiano hayo, Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema kwa kila anayecheza bahati nasibu yao, lazima ajiandae kulala masikini na kuamka tajiri.

  Alisema ushindi wa Biko ni rahisi kwa wale wanaocheza kwa kutumia mitandao ya simu ya M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money ambapo namba ya Kampuni ni 505050 na kumbukumbu ni 2456, huku kianzio cha kuchezea Biko kikianzia Sh 1,000 na kuendelea.

  “Mbali na kushinda Sh Milioni 20 kama alivyoshinda Chitanda na hatimae kumkabidhi fedha zake siku moja baada ya kushinda, pia Watanzania wanaweza kushinda zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, huku wanaocheza mara nyingi zaidi kwa kufanya miamala kwenye simu zao wakiwa na nafasi kubwa zaidi ya kushinda zawadi za papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya Jumatano na Jumapili kwa ajili ya kuwania donge nono la Sh Milioni 20,” Alisema.

  Naye Chitanda alisema kwamba fedha za Biko ni tamu inapotokea bahati ya ushindi, huku akisema amekubaliana na kauli mbiu ya Biko inayojulikana kama ushindi nje nje, kutokana na kuibuka kwake mshindi wa Sh Milioni 20 ambazo amekabidhiwa haraka.

  “Nimekubaliana kwa kiasi kikubwa na kauli mbiu hii ya ushindi nje nje, maana awali nilijua sitaweza kushinda, lakini kwa kushinda kwangu, naomba niwaambie Watanzania wote waendelee kucheza Biko washuhudie nguvu ya Buku inavyozalisha mamilioni,” Alisema Chitanda.
  Baada ya kukabidhiwa fedha zake pamoja na kupewa ushauri wa kifedha kutoka kwa wataalamu wa NMB, mshindi mwingine wa Biko wa Milioni 20 anatarajiwa kupatikana Jumapili hii kwenye droo ya 31.


  Mshindi wa Biko droo ya 30, Anthony Chitanda, akionyesha shangwe zake baada ya kupokea fedha zake Sh Milioni 20 kutoka Biko kama sehemu ya ushindi wake.

  Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Bahati Nasibu ya Biko, Hassan Melles kulia amkabidhi mshindi wao wa droo ya 30 Anthony Chitanda katikati katika benki ya NMB, Tawi la Bank House, Posta, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa wa NMB. Makabidhiano hayo yalifanyika jana mchana.
  Mshindi wa droo ya 30 Biko Ijue Nguvu ya Buku, Anthony Chitanda kushoto akiwa na mke wake baada ya kukabidhiwa hundi ya fedha zake Sh Milioni 20 saa chache kabla ya kuelekea benki ya NMB, Posta jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukabidhiwa fedha zake jana.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Mshindi wa Milioni 20 za Biko Kimara Suka akabidhiwa fedha zake Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top