728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, August 11, 2017

  JAFO: ZOEZI LA HOSPITALI TEMBEZI LIFANYIKE MIKOA YOTE

  NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amewaagiza Makatibu tawala wa mikoa yote Tanzania bara kuratibu zoezi la Hospitali tembezi katika mikoa yao ili kuwasaidia wananchi wa hali ya chini kupata huduma ya kibingwa. 

  Jafo ametoa agizo hilo leo alipokuwa akizindua huduma za hospitali tembezi kwa wilaya ya Chemba na Kondoa zoezi ambalo limefanyikia mjini Kondoa.Mpaka sasa zoezi hilo limeshafanyika katika wilaya ya Kongwa, Mpwapwa, Chamwino na sasa linaendelea kwa wilaya za Chemba na Kondoa.

  Akizindua huduma hiyo, Jafo ameumwagia sifa uongozi wa mkoa wa Dodoma kwa kuratibu vyema zoezi hilo ambapo zaidi ya wagonjwa 8,000 wamefanyiwa uchunguzi huku 500 wakifanyiwa upasuaji mdogo na mkubwa.

  Amewataka wananchi wa wilaya hizo kujitokeza kwa wingi kupata huduma hizo za kibingwa huku akiwataka kupima tezi dume kwa kuwa umekuwa ugonjwa tishio kwa wanaume.

  Ameeleza kuwa huduma hizo za kibingwa zinatolewa kwa gharama nafuu na hivyo kuwawezesha wananchi wasio na uwezo kupata matibabu.Jafo amewapongeza madaktari bingwa wa mkoa wa Dodoma kwa kazi kubwa wanayoifanya na amewataka wengine waige mfano wa Dodoma.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi wa Hospitali tembezi katika wilaya ya Kondoa na Chemba.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk.James Kiologwe na viongozi wa wilaya ya Chemba na Kondoa.
  Mbunge wa Chemba Juma Nkamia akizungumza katika uzinduzi wa Hospitali tembezi katika wilaya za Kondoa na Chemba.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wagonjwa na viongozi katika uzinduzi wa Hospitali tembezi.
  Wananchi waliofika katika uzinduzi wa hospitali tembezi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: JAFO: ZOEZI LA HOSPITALI TEMBEZI LIFANYIKE MIKOA YOTE Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top