728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, July 8, 2017

  Waziri wa usalama wa Kenya Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery afariki dunia.  Jenerali Joseph Ole Nkaissery enzi za Uhai wake.
   
  Waziri huyo amefariki dunia saa chache baada yake kulazwa katika hospitali ya kibinafsi ya Karen kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu. 
  Taarifa za kifo chake zimetangazwa na mkuu wa utumishi wa umma Bw Joseph Kinyua mwendo wa saa kumi na moja alfajiri. 

  “Ni kwa huzuni kubwa na mshangao kwamba tunatangaza kifo cha ghafla cha Waziri wa Usalama wa Ndani Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery,” taarifa ya Bw Kinyua imesema. 

  “Taifa litaendelea kupashwa habari zaidi punde maelezo yatakapopatikana.” 
  Jenerali Nkaissery amefariki siku chache baada ya mwanasiasa mkongwe G.G Gitahi aliyekuwa seneta wa jimbo la Laikipia kufariki dunia.
  Waziri wa elimu nchini Kenya Dkt Fred Matiang'i (pichani) ameteuliwa kuwa kaimu waziri wa usalama wa ndani kufuatia kifo cha aliyekuwa waziri Meja Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Waziri wa usalama wa Kenya Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery afariki dunia. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top