728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, July 26, 2017

  WAZIRI MWAKYEMBE ATOA SHUKRANI KWA WADAU MBALIMBALI KUFUATIA KIFO YA MKEWE MAREHEMU LINAH MWAKWEMBE

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo katika picha) leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa neno la shukrani kwa wote walioshiriki katika kumfariji kipindi cha msiba wa mke wake mpendwa Bi. Linah George Mwakyembe.

  Napenda kutumia fursa hii kwanza kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa neema na baraka zake na pili kutoa shukrani zangu za dhati kwa Watanzania wote kwa upendo na ushirikiano mkubwa mlionipa mimi na familia yangu katika kuomboleza kifo cha mke wangu mpendwa Bi.Linah Widmel-George Mwakyembe na baadaye katika mazishi yake wilayani Kyela.

  Familia inapenda kutoa shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli; Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan; Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, na Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai kwa mchango wao mkubwa katika kumuuguza marehemu wakati wa uhai wake.

  Aidha, familia inawashukuru viongozi hao waandamizi wa nchi pamoja na Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, Naibu Spika, Mhe. Tulia Ackson Mwansasu, wake wa viongozi, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, viongozi wetu wa nchi wastaafu, Wabunge, Majaji, Mabalozi wa nchi mbalimbali, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Maaskofu wa Kanisa la Kiluteri, Makanisa ya Moravian na makanisa ya kiroho (Mito ya Baraka, Living Water, Evangelical Brotherhood nk) kwa ushirikiano wao katika maombolezi na mazishi ya marehemu.

  Wana-familia tutakumbuka daima moyo adhimu wa upendo na ushirikiano tulioupata toka kwa Katibu wa Bunge na maafisa wake, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na timu yake mzima ya Wizara, Makatibu Wakuu wakiongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi, watendaji wakuu wa taasisi, asasi na kampuni mbalimbali, na wananchi wote kwa ujumla katika kipindi hicho kigumu.

  Pia napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru Wana-Kyela wote kwa uvumilivu waliouonesha kipindi chote cha kumuuguza marehemu na ushirikiano wao wa dhati katika mazishi yake.

  Mwisho lakini si kwa umuhimu, nawashukuru sana madaktari na wauguzi waliomhudumia marehemu kwa kujituma, kwa weledi na ustahimilivu wao ili kuokoa maisha yake lakini Mungu akampenda zaidi. Vilevile wamiliki wa vyombo vya habari, waandishi na watangazaji kwa kukesha nasi kipindi chote cha msiba Dar es

  Salaam na Kyela wakitekeleza wajibu wao wa kitaaluma na vilevile kutufariji wafiwa kwa hali na mali.

  Nawaomba wote mpokee shukrani zangu za dhati na Mwenyezi Mungu awabariki kwa moyo wa ushirikiano na upendo mliouonyesha kwetu.

  Bwana alitoa na Bwana Ametwaa, jina lake lihimidiwe.

  Dkt. Harrison George Mwakyembe (Mb),
  WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO,
  26/07/2017.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAZIRI MWAKYEMBE ATOA SHUKRANI KWA WADAU MBALIMBALI KUFUATIA KIFO YA MKEWE MAREHEMU LINAH MWAKWEMBE Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top