728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, July 14, 2017

  WAZIRI MKUU ATEMBELEA MRADI WA KUSAFIRISHA UMEME LINDI

  * Asema changamoto ya kukatika umeme Mkoa wa Lindi kuwa historia 
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema changamoto ya kukatika umeme katika mkoa wa Lindi kuwa historia baada ya kukamilika kwa mradi wa kusafirisha umeme wa kilovolti 132 Mtwara-Lindi.   
                            
  Amesema hayo leo (Alhamisi, Julai 13, 2017) alipotembelea mradi huo wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi. 
  Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa mradi huo uliogharimu sh. bilioni 16 kutamaliza changamoto ya upatikanaji wa umeme katika mkoa wa Lindi. 
  Amesema mkakati wa Serikali ni kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme ili Watanzania wapate umeme mwingi utakaosambazwa hadi vijijini kwa gharama nafuu. 

  “Mikoa wa Lindi ulikuwa na shida kubwa ya kukatika kwa umeme, kukamilika kwa mradi huu ni mkombozi kwetu, tunawakaribisha wawekezaji waje kuwekeza kwa sababu sasa tunanishati ya uhakika.”
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof. James Mdoe, wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne (katikati) ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Mnauye.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea maelezo ya mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi kutoka kwa Mhandisi Jafary Msuya, wakati alipotembelea mradi huo unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea maelezo ya mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi kutoka kwa Mhandisi Ferdinand Mwinje,wakati akikagua mradi huo unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiongea na wananchi, wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme wa Mahumbika, unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)​
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAZIRI MKUU ATEMBELEA MRADI WA KUSAFIRISHA UMEME LINDI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top