728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, July 26, 2017

  SHAFFIH DAUDA NA WENZAKE WAHOJIWA NA TAKUKURU KWA TUHUMA ZA RUSHWA JIJINI MWANZA,WAACHIWA KWA DHAMANA

  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Mwanza (TAKUKURU) imethibitisha kuwahoji wanafamilia wa soka wakiwemo Mjumbe Chama cha Soka Wilaya ya Ubungo (UFA) Shaffih Dauda na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam (DRFA) Almas Kasongo.

  Mbali na hao TAKUKURU wamethibitisha pia kuwahoji Elias Mwanjali, Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Mwanza, Leonard Malongo, Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Mbeya Bw. Elias Mwanjaa , Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Mguu mkoa wa Shinyanga Benasta Lugola na wajumbe wa mikoa ya jirani kwa sababu ya kuwepo kwa viashiria vya rushwa na kampeni.

  Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Mwanza Mhandisi Ernest Makale amethibitisha kuwahoji kwa wanafamilia hao wa mpira ambapo waliwashikilia tokea jana saa 3 usiku na wameachiwa kwa dhamana huku uchunguzi ukiendelea na watakapojiridhisha wanaweza kuwakamata tena.

  Taarifa inasema kuwa wanafamilia hao walitumia mgongo wa Ndondo Cup kufanya jambo lao usiku wa saa 3 jana na ndipo walipotiliwa shaka na kufuatiliwa na kutiwa mikononi mwa Takukuru ambao wamethibitisha kuwashikilia tokea jana usiku na kuwaachia kwa dhamana

  Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Mwanza Mhandisi Ernest Makale.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SHAFFIH DAUDA NA WENZAKE WAHOJIWA NA TAKUKURU KWA TUHUMA ZA RUSHWA JIJINI MWANZA,WAACHIWA KWA DHAMANA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top