728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, July 26, 2017

  NYUMBA ZA KULALA WAGENI PAMOJA NA KUMBI ZA STAREHE ZILIZO KARIBU NA MAENEO SHULE ZIVUNJWE - RC MAKONDA

  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri katika jiji la Dar es Salaam ndani ya siku 20 kusiwepo nyumba za wageni pamoja na kumbi za starehe katika maeneo yanayozunguka shule.

  Makonda ameyasema hayo wakati akizungumza na wakuu wa shule za sekondari na Msingi uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es salaam. ambapo amesema kuwa  shule ni kwa ajili ya kutoa elimu hivyo kuwepo kwa vitu hivyo vinafanya kuhalibu na kuwahadaa wanafunzi.

  Amesema kuwa maeneo yote ya shule yapimwe ili kusiwepo kwa mazingira ya kuweza watu kufanya kujenga maeneo hayo.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na maafisa elimu, waalimu wakuu shule za sekondari na msingi leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa akizungumza na katika Mkutano wa Walimu Wakuu Shule za Sekondari na Msingi leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Shule Kisarawe 11, Elieshi Emmanuel akizungumza katika Mkutano wa Wakuu wa Shule juu.
  Mkutano ukiendelea.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: NYUMBA ZA KULALA WAGENI PAMOJA NA KUMBI ZA STAREHE ZILIZO KARIBU NA MAENEO SHULE ZIVUNJWE - RC MAKONDA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top