728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, July 31, 2017

  MSAFARA WA MAGARI YA KIZAMANI KUANZA ZANZIBAR


  Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Rashid Ali Juma mwezi ujao,anatarajia kuzindua msafara wa magari ya zamani mjini humo ili kuamsha aina mpya ya utalii.

  Msafara huo unatarajiwa kuanzia Hyatt Park hoteli iliyopo mjini Zanzibar na kumalizikia Melia hoteli Kiwengwa.

  Waziri Juma amesema hayo leo na kuongeza kuwa lengo la safari hiyo ni kuamsha aina mpya ya utalii itakayopelekea watalii wengi kuja nchini.

  Amesema magari hayo ya miaka ya 60 yalikuwa yakitumiwa na wafalme na masultani, lakini hadi leo yanaweza kutembea."Utalii unachangia pato la Zanzibar kwa asilimia 27 huku ukichangia asilimia 80 ya fedha za kigeni kwani mambo mengi ya kitalii yamekuwa ya kawaida".

  Amesema kwa kushirikiana na Hyatt hoteli tumekuja na mbinu mpya ya kuwavutia watalii wengi zaidi.Amesisitiza kuwa hakutakuwa na mbio za magari bali ni msafara wa magari hayo ya zamani ambayo yatatembea umbali wa kilomita 30 na kwa kuanzia yatakuwa magari sita, matatu ya watu binafsi na matatu ya Hyatt.

  Aidha amewahakikishia usalama wa kutosha katika msafara huo ambapo vyombo vya ulinzi vitakuwa vikisindikiza mwanzo mpaka mwisho wa safari.
  Nae Meneja mkuu wa Hyatt hoteli Garry Friend alisema msafara huo utaanzia Hyatt park hoteli Zanzibar ukipitia mji mkongwe na kumalizikia Melia Kiwengwa Agosti 26 ambayo ndiyo siku ya ufunguzi rasmi. 

  Amesema lengo la kutumia magari hayo yaliyotumika miaka ya 60 ni kusisimua utalii."Watu wengi watavutiwa na aina hii ya utalii" alisema Friend.
   Waziri wa Habari utalii Utamaduni Sanaa na Michezo Mh.Rashidi Juma Kushoto Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema Jijini Leo
  Kulia ni Meneja Mkuu wa Hyat Hotel Bwn Garry Friend
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MSAFARA WA MAGARI YA KIZAMANI KUANZA ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top