728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, July 3, 2017

  Meya wa Jiji la DSM Mwita awataka wananchi kuwa wamoja bila kujali itikadi ya vyama vyao.

  NA CHRISTINA MWAGALA ,OFISI YA MEYA WA JIJI

  MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema watanzania hawajafikia hatua ya kubaguana kwa kiitikadi ya vyama, Dini, Kabila badala yake wote wanapaswa kutangaza hali ya Umoja, Upendo na Mshikamano katika nchi yao.

  Meya Mwita alitoa kauli hiyo jijini hapa jana, wakati wa harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa Kanisa la kisasa la Tanzania Assemblies Of God (TAG) lililopo Kivule ,Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini hapa ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa watanzania wanapaswa kuwa wamoja ili nchi iendelee kuwa na amani.

  Alisema yapo mambo mbalimbali ambayo yanajitokeza ndani ya nchi ambapo kama watanzania , kwakushirikiana na viongozi wa dini kwa pamaoja wanapaswa kusimama na kuliombea Taifa ili kuendelea kudumisha amani iliyopo.

  " Tangu nimezaliwa sijawahi kushuhudia vita, machafuko katika nchi yetu, kikubwa huwa naona amani iliyotawala, Upendo, na umoja , sasa nawasishi sana ndugu zangu tuendelee kuwa wamoja tusibaguane, kwa namna yoyote ile , ili nchi yetu iendelee kuwa na amani" alisema Meya Mwita.

  "Baba wataifa Hayati Mwalim Julius Nyerere enzi ya uhali wake alikuwa akisisitiza sana kulinda amani ya nchi yetu, na sisi ambao tupo hai hadi sasa , mambo ya vyama, Udini, Ukabila tuweke pembeni tusimame kama Taifa moja.

  Awali akijibu risala iliyoandaliwa na uongozi wa kanisa hilo, Meya Mwita aliahidi kuchangia katika ujenzi huo mifuko 100 ya Simenti na kiasi cha Fedha shilingi 500,000 huku aliwataka waumini wa kanisa hilo kujitolea ili kufanikisha ujenzi huo.

  Risala hiyo ilieleza kujenga kanisa la kisasa lenye uwezo wa kuchukua waumini 600 ambapo jumla ya shilingi milioni 95 zinahitajika ili kukamilisha ujenzi huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Meya wa Jiji la DSM Mwita awataka wananchi kuwa wamoja bila kujali itikadi ya vyama vyao. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top