728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, July 13, 2017

  MBUNGE WA CHADEMA AWAOMBA WANANCHI WALIOMBEE TAIFA AMANI

  MBUNGE viti Maalumu Chadema, Mheshimiwa Upendo Peneza amewaomba wananchi waliombee Taifa liendelee kuwa na amani pamoja na kuwaombea viongozi wa kisiasa wawe na uvumilivu ili wazidi kusonga mbele kimaendeleo.

  Aliyasema hayo jana (Jumatano, Julai 12, 2017), katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa shule ya msingi Likangara wilayani Ruangwa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mkoani Lindi.

  “Wananchi wa Ruangwa nawatakia maisha mema ili mzidi kusonga mbele, tuombee amani ya nchi yetu na mtuombee viongozi tuwe na uvumilivu wa kisiasa.”

  Mbali na Mheshimiwa Upendo, pia mkutano huo uliudhuriwa na wabunge wengine ambao ni Mheshimiwa Hassan Masala (Nachingwea), Mheshimiwa Zubery Kuchauka (Liwale), Mheshimiwa Hassan Kaunje (Lindi Mjini) na Mheshimiwa Hamida Abdalaah (Viti Maalumu).

  Kwa pamoja wabunge hao walisema lengo la kushiriki kwenye ziara hiyo ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano katika kuwaletea wananchi maendeleo.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi aliwataka wananchi wa mkoa huo kuhakikisha wanaendelea kudumisha na kuilinda amani iliyoko kwa sababu ndiyo inayowawezesha kufanya shughuli zao za kimaendeleo.

  Alisema licha ya kuwepo kwa matukio machache ya uhalifu yanayojitokeza katika baadhi ya maeneo vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na mikoa jirani limejizatiti kukabiliana na wahalifu wa aina yoyote kwa mtu mmoja mmoja au vikundi.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa viti Maalumu Chadema, Mheshimiwa Upendo Peneza, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MBUNGE WA CHADEMA AWAOMBA WANANCHI WALIOMBEE TAIFA AMANI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top