728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, July 3, 2017

  MAONESHO YA SABASABA 2017; PPF WAJIZOLEA SIFA YA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANACHAMA NA WANANCHI WANAOTEMBELEA BANDA HILO

   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio, (mwenye suti), akiungana na wafanyakazi wenzake kuhudumia wananchi wakati wa maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa uya Dar es Salaam leo Julai 2, 2017. Wananchi wengi waliotembelea banda hilo wamefurahishwa na huduma zitolewazo na wafanyakazi wake kwa kwa jinsi wanavyosikiliza na kutoa huduma kwa wanachama na wananchi wengine. miongoni mwa maswali mengi yaliyoulizwa mara kwa mara ni kuhusu mpango wa uchangiaji wa hiari ujulikanao kama "Wote Scheme), unaotoa fursa kwa wajasiriamali wadogo kama mama lishe madereva wa bodaboda, wamachinga na mtu yeyote anayefanya kazi halali ya kumuingizia kipato anavyoweza kujiunga na mpango huo na hatimaye kupata faida mbalimbali ikiwemo bima ya afya na mikopo kwa wajasiriamali wadogo,
   Wananchi wakipatiwa maelezo kuhusu shughuli na huduma zitolewazo na PPF.
   Meneja wa elimu kwa wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. Kwame Temu, (kushoto), akitoa maelezo kwa mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere kuinakofanyika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam leo Julai 2, 2017
    Wananchi wakipatiwa maelezo kuhusu shughuli na huduma zitolewazo na PPF.
    Wananchi wakipatiwa maelezo kuhusu shughuli na huduma zitolewazo na PPF.
   Wafanyakazi wa PPF, wakiwa makini katika kuwahudumia wananchi waliofika banda la Mfuko huo   Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (kushoto), akizungumza jambo, wakati alipokutana na muigizaji mkongwe hapa nchini, Mzee Jangala, (wapili kushoto), wakati akitembelea bustani daraza ya Jeshi la Magereza, kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, leo Julai 2, 2017. Wengine pichani kutoka kulia ni Bi. Yunge Saganda wa Jeshi la Magereza, Bi. Lulu Mengele, Meneja Uhusiano wa PPF na Bi Jannet Ezekiel Afisa Uhusiani Mwandamizi wa Mfuko huo
  Mama Anna Mkapa, (kushoto),  ambaye ni  Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote, (EOTF), na Mke wa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (wapili kushoto), Mama Mwantumu Mahiza, wakati alipotembelea banda la EOTF linalowakusanya wajasiriamali mbalimbali kuitoka nchini kote leo Julai 2, 2017
   Mjasiriamali kutoka mkoani Kigoma, Bi.Dporothy Timoth Takwe, (kushoto), akitoa maelezo ya ladha nzuri ya dagaa wa ziwa Tanganyika, wakati mama Mkapa, Mkurugenzi Mkuu wa PPF na mmoja wa viongozi wa televisehni ya Agape, (kulia), wakati walipotembelea banda la mjasiriamali huyo lililoko jengo la EOTF
   Mama Mkapa, Mkurugenzi Mkuu Erio, wakitazama bidhaa zilizofungwa vizuri na wajasiriamali wa Tanzania
  Bw. Erio akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Magereza
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MAONESHO YA SABASABA 2017; PPF WAJIZOLEA SIFA YA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANACHAMA NA WANANCHI WANAOTEMBELEA BANDA HILO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top