728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, July 12, 2017

  MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AMRITHI MAMA SALMA KIKWETE ULEZI WA TANZANIA GIRL GUIDES

  Na Abraham Ntambara. 

  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wasichana ambo ni wanachama wa chama cha Tanzania Girl Guides Association (TGGA) kuzingatia mafunzo wanayopatiwa kwa ajili ya maisha yao ya baadaye. 

   Kauli hiyo aliitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akikabidhiwa kijiti cha kuwa mlezi wa chama hicho kutoka kwa Mama Salma Kikwete anayesitaafu nafasi hiyo aliyoihudumu kwa zaidi ya miaka 12.

   “Niwatake tu watoto wangu kutochukulia kwa mzaha mafunzo mnayopatiwa kwani ni tija kwa maendeleo ya Taifa,” alisema Makamu wa Rais. 
  Aidha aliwaahidi wanachama kutowaangusha katika kutekeleza majukumu ya kukilea chama hicho ambapo alimpongeza Mama Salma Kikwete kwa kuweza kukiongoza vizuri kwa mafanikio makubwa licha ya kuwa na majukumu mengine.
  Aliyekuwa Mlezi wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Mama Salma Kikwete (kushoto) akimkabidhi  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan bendera ikiwa ni ishara ya kumpatia ulezi wa chama hicho katika hafla iliyofanyika, kwenye viwanja vya Jumba la Makumbusho Dar es Salaam leo
  Mama salma akimkabidhi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mpango mkakati wa TGGA
  Samia Suluhu Hasan akimkabidhi Mlezi mstaafu wa TGGA zawadi ya saa aliyopewa zawadi na uongozi wa TGGA kwa ajili ya kumbukumbu.

  Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi
  Salma Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba
  Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamishna wa TGGA

  Samia akiangalia kazi mbalimbali zinazofanywa na Girl Guides

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AMRITHI MAMA SALMA KIKWETE ULEZI WA TANZANIA GIRL GUIDES Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top