728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, July 14, 2017

  DC.MNDEME AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA NA KUVIFUNGIA VITUO NANE VYA MAFUTA AKISHIRIKIANA NA TRA DODOMA MJINI LEO -

  Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Mh.Christina Mndeme leo amefanya ukaguzi kwenye vituo vya mafuta ili kuona kama wafanyabiashara ya kuuza mafuta wanafuata sheria na taratibu za utoaji risiti na ulipaji kodi kwa kufunga mashine sahihi ya utoaji risiti iliyofungwa moja kwa moja kwenye pampu au mita ya mafuta. 

  Katika ZIARA hiyo Kati ya vituo 9 alivyovitembelea amegundua kituo kimoja tu ndiyo kinafuata sheria na kuchukua hatua ya kuvifungia vituo nane (08).

  Kazi hiyo imefanyika kwa kushirikiana na maafisa wa TRA Dodoma Mjini. Tunatekeleza kwa Hapa Kazi Tu, Lipa kodi kwa Maendeleo ya Taifa letu.

  Pichani kushoto ni  Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Mh.Christina Mndeme akishirikiana na Ofisa wa TRA kukifungia moja ya kituo cha mafuta mkoani humo kilichobainika kutofuata sheria na taratibu za utoaji risiti na ulipaji kodi kwa kufunga mashine sahihi ya utoaji risiti iliyofungwa moja kwa moja kwenye pampu au mita ya mafuta.
  Wasimamizi wa kituo wakipewa maelekezo baada ya kituo chao cha mafuta kufungiwa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: DC.MNDEME AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA NA KUVIFUNGIA VITUO NANE VYA MAFUTA AKISHIRIKIANA NA TRA DODOMA MJINI LEO - Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top