728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, June 2, 2017

  Vijana wampongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kushitukia unyonyaji uliokuwepo katika sekta ya Nishati na Madini


  Na Ashraf Said, Globu ya Jamii .

  Vijana wazalendo wampongeza Rais, Dk. John Pombe Magufuli juu ya hatua stahiki anazoendelea kuchukua dhidi ya unyonyaji uliokithiri katika sekta ya Nishati na Madini.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa vijana hao, Mwita Nyarukururu amesema jitihada za Rais Dk. John Pombe Magufuli zinawapeleka watanzania katika uchumi wa kati wa nchi kuweza kujitegemea na kuachana na wanyonyaji wa rasilimali katika sekta ya nishati na madini kutokana na misaada wanayoitoa .

  Amesema kuwa Rais Dk. John Pombe Magufuli ameonyesha dhamira ya kweli katika kuhakisha watendaji waliopewa mamlaka wanawajibika na wanaposhindwa kufanya hivyo hatua zinachukuliwa alivyoweza kuiwajibisha Wizara ya Madini pamoja na Bodi ya Ukaguzi wa Madini (TMAA).

  “Unyonyaji na Uhujumu uchumi katika sekta ya madini umekuwa ukipigiwa kelele na wananchi kutokana na Mikataba kuwa ya siri na mibovu isiyonufaisha Taifa,”Amesema.

  Aidha wamemuomba Rais Dk. John Pombe Magufuli na Serikali yake kupeleka upya bungeni mswada wa sheria zote zinazohusu sekta ya Nishati na Madini kwa lengo la kujadiliwa upya kwa maslahi ya taifa na wananchi wote.

  Mwenyekiti wa vijana Vijana Wazalendo, Mwita Nyarukururu katikati akizungumza na waandishi wa habari juu hatua ambazo anazichukua Rais Dk. John Pombe Magufuli katika sekta ya Nishati na Madini leo jijini Dar es Salaam. Kushoto Halima Makoroganya kulia ni Rose Manumba
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Vijana wampongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kushitukia unyonyaji uliokuwepo katika sekta ya Nishati na Madini Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top