728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, June 1, 2017

  SHUWASA YAKUTANA NA WADAU WA MAJI KUJADILI MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA  Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) imekutana na wadau wa huduma ya maji kujadili rasmu ya Mkataba wa Huduma Kwa Wateja ambapo mkataba utakaopitishwa na wadau utaanza kutumika kuanzia Julai Mosi ,2017.

  Warsha ya kujadili mkataba wa huduma kwa wateja imefanyika leo Jumatani June 1,2017 katika ukumbi wa Vijana Center Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro.

  Akizungumza katika warsha hiyo,Matiro aliwataka wadau wa maji kujadili rasmu hiyo kwa umakini zaidi ili kuweka mambo ya msingi ambayo yatapunguza malalamiko kutoka wateja ikiwemo ongezeko la bei ya maji kwa watumiaji wa majumbani.

  Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Reuben Mwandumbya alisema kutokana mamlaka hiyo kuwajali wateja wake imeona ni vyema kukutana na wadau ili kujadili mkataba mpya wa huduma kwa wateja.
   
  “Mkataba uliokuwepo umemaliza muda wake hivyo tumeleta kwenu rasmu ya mkataba ili tujadili kwa pamoja tuweze kuboresha zaidi huduma ya maji kwa wateja wetu”,alieleza Marco

  Miongoni mwa wadau walioshiriki katika warsha hiyo ni meya wa manispaa ya Shinyanga,madiwani,viongozi wa dini,viongozi wa taasisi mbalimbali,watendaji wa kata,wenyeviti wa serikali za mitaa,waandishi wa habari na wadau mbalimbali.

  Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufungua warsha/kikao cha kujadili rasmu ya huduma kwa wateja

  Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akizungumza katika warsha hiyo.Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA,Deogratius Sulla,kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Reuben Mwandumbya

  Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga ,Josephine Matiro akizungumza katika warsha ya wadau wa maji manispaa ya Shinyanga

  Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga ,Josephine Matiro akisisitiza jambo katika warsha hiyo .

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Reuben Mwandumbya akielezea umuhimu wa wadau wa maji kujadili rasmu ya mkataba wa huduma kwa wateja

  Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA,Deogratius Sulla akizungumza ukumbini

  Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Agnes Machiya akizungumza katika warsha hiyo

  Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Agnes Machiya akizungumza

  Afisa Uhusiano wa SHUWASA,Nsianeli Gelard akielezea kuhusu mkataba wa huduma kwa wateja


  Afisa Uhusiano wa SHUWASA,Nsianeli Gelard akiendelea kuelezea kuhusu mkataba wa huduma kwa wateja

  Afisa Rasilimaliwatu na Utawala wa SHUWASA,Kambira Mtebe akifafanua kuhusu mktaba wa huduma kwa wateja

  Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii manispaa ya Shinyanga,Hassan Mwendapole akiongoza majadiliano wakati wa warsha hiyo

  Warsha inaendelea

  Warsha inaendelea
  Diwani wa kata ya Ndembezi (CCM) David Nkulila akichangia hoja katika warsha hiyo

  Diwani wa viti maalum kata ya Shinyanga Mjini,Zenna Gulam (Chadema) akichangia hoja .

  Mchungaji Obeid Jilala ambaye pia ni diwani wa kata ya Lubaga (Chadema) akichangia hoja ukumbini

  Wajumbe wakiwa ukumbini

  Warsha inaendelea

  Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini

  Wajumbe wakiwa ukumbini

  Wadau wakiwa ukumbini


  Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SHUWASA YAKUTANA NA WADAU WA MAJI KUJADILI MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top