728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, June 5, 2017

  SHIRIKA LA ANGA LA ETIHAD KUTOA OFA ZA BURE KWA ABIRIA WAKE WA DARAJA LA UCHUMI WA MASHARIKI YA KATI, AFRIKA NA PAKISTAN AbuDhabi.

  Shirika kuu la anga la Umoja wa nchi ya falme za kiarabu litatoa nafasi kwa abiria wake kutoka mashariki ya kati, Afrika na Pakistan kupumzika katika hoteli ya Raddison Blu jijini Abu Dhabi kisiwani Yas. Fursa hii imeanza rasmi hivi karibuni na kumalizika tarehe 15, Novemba 2017.

  Mohammad Al Bulooki, Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa shirika la anga la Etihad alisema “Shirika la Etihad lina furaha kuwaalika wageni wote kuja kuliona na kulifahamu katika mji wa Abu Dhabi kwa macho yao wenyewe. Jiji hilo kuu la Umoja wa falme za Kiarabu lina mengi ya kuwaonesha abiria wote wanaosafiri endapo wanavutiwa na utamaduni, kupumzika sehemu mbali mbali kama visiwa vya bahari, michezo nk.

  Kama shirika la ndege la kitaifa la Etihad ni sehemu muhimu ya jiji hili zuri na wote wanaosafiri kupitia Abu Dhabi wanatakiwa kuhamasishwa kuja kujionea uzuri wa jiji hili. Ofa hii ni kwa wateja ili waweze kutenga muda wao na kuja kutembelea vivutio mbalimbali vya Abu Dhabi wakiwa katika safari zao. Kutembelea jangwa hilo zuri pamoja na msikiti mkubwa wa sheikh Zayed, moja kati ya misikiti mikubwa sana duniani, kuembelea vivutio mbalimbali vya kisiwa cha Yas, na kupata nafasi ya kufurahia kwa mara ya kwanza katika hoteli kubwa za kitalii duniani.

  Zaidi ya wageni milioni 4.4 walirekodiwa kutembelea jiji la Abu Dhabi mwaka 2016 na kuthibitisha kuwa Umoja wa falme hizo za kiarabu ni moja kati ya vivutio vingi vya wasafiri wanaopitia hapo wakati wanaposafiri. Wageni wanaweza kujipatia fursa hii kuzifahamu vivutio vya burudani mbalimbali maarufu kibiashara ikiwemo pwani za bahari zenye mchanga mweupe, hifadhi zenye mandhari tofauti kama Yas Waterworld na Ferrari World, jangwa la misafara ya safari   Sanaa, taasisi za kitamaduni kama Manarat Al Saadiyat na makumbusho ya Louvre yanayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni, sehemu nzuri za kitaifa na kimataifa za kupata chakula, sehemu za kucheza mchezo wa golf kimataifa, na kanuni ya 1 ya shirika la Etihad ya kufuatilia mbio kubwa Zaidi jijini Abu Dhabi.

  Jiji la Abu Dhbi pia linatoa nafasi kupata sehemu mbalimbali za kununua mahitaji ya kila aina kuweza kukidhi mahitaji yao. Jiji hilo linajivunia maduka makubwa kama Yas, Abu Dhabi, Marina na Galleria- moja kati ya sehemu kubwa za kifhari za kununa mahitaji.

  Shirika la ndege la Etihad limekua na programu ya kupitisha wasafiri wake sehemu mbali mbali wakiwa safarini kuanzia mwaka 2011, na kutoa huduma mbali mbali ikiwa nia pamoja na kukutana viwanja vya ndege, na kusaidia usafiri, mahala pa kupumzikia, ziara mbali mbali na huduma za upatikanaji wa hati za kusafiria
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SHIRIKA LA ANGA LA ETIHAD KUTOA OFA ZA BURE KWA ABIRIA WAKE WA DARAJA LA UCHUMI WA MASHARIKI YA KATI, AFRIKA NA PAKISTAN AbuDhabi. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top