728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, June 20, 2017

  NEWS ALERT: SHABIKI WA YANGA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI

  Globu ya Jamii imepokea taarifa ya kifo cha shabiki maarufu wa timu ya Yanga Ally Mohamed almaarufu kwa jina la Ally Yanga. Taarifa zinaeleza kuwa Ally Yanga amefariki Dunia mapema leo katika ajali ya gari eneo la kijiji cha Chipogoro wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.  Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi-Amin.

  UPDATES. 

  Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa amethibitisha kifo cha aliyekuwa shabiki maarufu wa klabu ya soka ya Yanga Ally Yanga kilichotokea leo katika ajali ya gari aina ya Rav4 eneo la Chipogolo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

  Ally Yanga ambaye pia ni mkereketwa wa Mwenge wa Uhuru alikutwa na mauti akiwa katika gari la kampuni ya Faidika ambalo lilikuwa kwenye shughuli zake za promosheni na SIO KWAMBA alikuwa kwenye msafara wa Mwenge kama inavyoenezwa.

  Ally aliyezaliwa mkoani Shinyanga Machi 1, mwaka 1984 katika familia ya watoto sita, kabla ya umauti wake inafahamika alikuwa anaishi Yombo Vituka, Dar es Salaam.

  Lakini tangu baada ya uchaguzi Mkuu Novemba 2015, Ally Yanga ameadimika viwanja vya soka kutokana na kujikita zaidi kwenye shughuli za Chama cha Mapinduzi CCM.
  Pichani juu na chini ni gari iliyopelekea kifo cha Shabiki huyo wa Yanga,Ally yanga
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: NEWS ALERT: SHABIKI WA YANGA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top