728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, June 28, 2017

  NCAA KUSHIRIKIANA NA TFF KUKUZA SOKA LA TANZANIA

   
  Naibu Mhifadhi (Huduma za Shirika) wa Mamlaka ya  Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Asangye N. Bangu, akipeana mkono na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa TFF wa Maendeleo ya Soka (TFDF), Derek Murusuri. Bw Bangu alizitembelea ofisi za TFDF ili kujadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano kati ya Mamlaka yake na Mfuko huo. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi za TFDF zilizoko Mikocheni jijini Dar Es Salaam leo (28 June 2017).

  Katika mazungumzo hayo, Bw Bangu ameahidi kushirikiana na Mfuko huo katika kuendeleza soka la Tanzania. Timu ya Taifa ya vijana walio chini ya miaka 20 (U-20), Ngorongoro Heroes, inatumia jina la Mamlaka hiyo ya Taifa ambayo pia ni mojawapo ya maajabu saba ya dunia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: NCAA KUSHIRIKIANA NA TFF KUKUZA SOKA LA TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top