728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, June 10, 2017

  Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson Awajulia Hali Watoto Wanawaosubiri kufanyiwa Upasuaji Wa Moyo Katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).


  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpokea Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanawaosubiri kufanyiwa upasuaji.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akieleza jinsi wanavyotoa huduma za matibabu ya magonjwa ya Moyo kwa Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanawaosubiri kufanyiwa upasuaji.
  Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimjulia hali mtoto Doreen Sostenes (3) ambaye Tulia Trust Fund imemlipia gharama za matibabu ya upasuaji wa Moyo ambao utafanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani.
  Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiwa amembeba mtoto Doreen Sostenes (3) ambaye Tulia Trust Fund imemlipia gharama za matibabu ya upasuaji wa Moyo ambao utafanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
  Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimtazama mtoto Johnson Raphael (6) akichora picha ya mtu wakati alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo ili kuwajulia hali watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji. Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani.
  Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiwa amembeba mtoto Zuwena Said (4) aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kusubiri upasuaji wa Moyo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani.
  Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimjulia hali mtoto Abdukarim Mahilo (2) aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kusubiri kufanyiwa upasuaji wa Moyo huku Mama wa mtoto Fatuma Bakari akiangalia.
  Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiongea na Maria Gervas ambaye ni mama wa Doreen Sostenes (3) anayelipiwa gharama za upasuaji wa Moyo na Tulia Trust Fund. Mhe. Dkt. Tulia alitembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.
  Daktari Bingwa wa Moyo kwa watoto na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo kwa Watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Sulende Kubhoja akimuelezea Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson magonjwa mbalimbali ya moyo yanayowasumbua watoto. Mhe. Dkt. Tulia alitembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.
  Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimbembeleza mtoto Venance Christopher (14) aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kusubiri upasuaji wa Moyo. Mhe. Dkt. Tulia alitembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.
  Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiongea jambo wakati akimjulia hali mtoto Rashid Kombo aliyelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) baada ya kufanyiwa upasuaji wa Moyo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani akifuatiwa na Daktari Bingwa wa Moyo kwa watoto na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo kwa Watoto Sulende Kubhoja.
  Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimsikiliza Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa Watoto na Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto Godwin Sharau alipotembelea leo chumba cha upasuaji wa Moyo kilichopo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwetwe (JKCI).

  Picha na JKCI
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson Awajulia Hali Watoto Wanawaosubiri kufanyiwa Upasuaji Wa Moyo Katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top