728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, June 13, 2017

  MBUNGE MLATA AHAMASISHA MICHEZO MASHULENI

  MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Singida,Marther Mlata amesema ili kukabiliana na utoro mashuleni pamoja na kusuasua kwa elimu,walimu hawana budi kutafuta namna ya kuwavutia watoto kupenda shule kupitia njia ya michezo.

  Mbunge Mlata alitoa ushawishi huo alipokuwa akiongea na wanafunzi,wazazi na walezi wa watoto wa shule ya sekondari ya Mtakatifu Vincent iliyopo katika Mji mdogo wa Mitundu,wilayani Manyoni,Mkoani Singida.

   “Ni lazima walimu mtafute namna ya kuwavutia watoto kupenda shule,kwa mfano michezo mtu mwingine anaweza akaenda shule kwa ajili ya michezo tu anasema shuleni huwa kuna mpira,huwa wanacheza ngoja niende”alifafanua Mlata ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida.

  Kwa mujibu wa Mlata mwanafunzi pindi anapokwenda shuleni kwa lengo la kushiriki katika michezo,inakuwa ni rahisi pia kumpata kwenye masomo darasani.

  Aidha Mbunge huyo aliweka bayana kwamba ili kuhakikisha michezo mashuleni inawezekana kuwepo kwa kipindi chote,alitumia hafla hiyo kukabidhi mipira kumi na jezi pea kumi kwa ajili ya kugawa katika shule zilizopo katika kata ya Mitundu.

  “Mimi sikuwa najua kwamba mmeongoza mmewafunga wanyiramba sisi wakimbu tumewafunga wale wanyiramba goli 3- 0 kwa hiyo nakuja kuhimiza michezo mashuleni”alibainisha Mbunge huyo mpenda michezo.

  Hata hivyo aliweka bayana kwamba ndiyo maana utoro mashuleni na kusuasua kwa elimu kunakochangiwa na wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata masomo alilazimika kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Itigi kuhakikisha anazisajili shule ambazo bado hazijasajiliwa ili kuwapunguzia watoto adha ya kutembea umbali huo mrefu.

  Ni Baadhi ya vifaa vya michezo vilivyotolewa msaada na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Singida,Marther Mlata kwa ajili ya kuhamasisha michezo katika shule zilizopo katika kata ya Mitundu,tarafa ya Itigi,wilayani Manyoni,Mkoani Singida wakati wa sherehe za Juma laa Taaluma lililoandaliwa na kata hiyo.(Picha Na Jumbe Ismailly)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MBUNGE MLATA AHAMASISHA MICHEZO MASHULENI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top