728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, June 28, 2017

  MAPOROMOKO YA MAJI MWALALO.

  Ni maporomoko yanayopatikana katika safu za milima ya LIVINGSTONE karibu na kingo za ziwa Nyasa (MATEMA BEACH), kijiji cha Matema, wilaya ya Kyela mkoani Mbeya. Mto huu humwaga maji yake ziwa Nyasa.

  Maporomoko haya yapo sehemu ambayo ni nzuri kwa (ku hike) ambapo huchukua takribani saa 1 (1hr) kutembea kwa mwendo wa kawaida (kwa miguu) kutoka katika kijiji cha Matema.

  Ni nzuri kutembelea eneo hilo kwa muda wa ziada pale unapotembelea fukwe za ziwa Nyasa kwaajili ya mapumziko au sababu za kitalii kwa ajili ya zoezi la mwili, moja kati ya interesting moment ni pale katika kakilima ka mwisho kanakohitaji kupanda kwa kujivuta katika kamba.

  Eneo lina sifa ya muonekano mzuri hasa wa rangi nyeupe ya maji yanayoporomoka katika miamba ya rangi ya mvuto ya kijivu.

  Maporomoko haya yametengeneza bwawa zuri na la asili katikati ya miamba (mawe) ambacho ni kizuri kwa kuogelea, na kupigia picha

  Ungependa kufika mahali hapa? Wasiliana na UYOLE CULTURAL TOURISM ENTERPRISE
  Simu 0783545464,
  Barua pepe: uyolecte@gmail.com
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MAPOROMOKO YA MAJI MWALALO. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top