728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, June 24, 2017

  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro katika wiki ya utumishi Simiyu

  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (Wa tatu kulia), akifuatilia taarifa ya utekelezaji iliyokuwa ikiwasilishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (Wa pili kulia) kabla ya kukutana na Watendaji wa Mkoa wa Simiyu ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mathias Kabunduguru.
  KIZ2
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Antony Mtaka (katikati) akimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia), alipokuwa akizungumza nae kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo katika mkoa wa Simiyu. Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
  KIZ3
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akiongea na Watendaji wa Mkoa wa Simiyu wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mathias Kabunduguru.
  KIZ4
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bw. Mariano Mwanyigu akitoa maoni wakati wa kikao kazi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.
  KIZ5
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akipata maelezo ya usindikaji maziwa kutoka kwa Mthibiti Ubora wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Gerald Baruti alipotembelea Kiwanda cha kusindika Maziwa (Meatu Milk) kilichoanzishwa na vikundi vya vijana kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.
  KIZ6
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akiangalia bustani ya Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, alipotembelea shughuli za maendeleo za Wilaya ya Meatu ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kushoto kwake ni Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bi. Upendo Naftali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro katika wiki ya utumishi Simiyu Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top