728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, June 15, 2017

  Kampuni ya Wazawa, yakamilisha hatua za Msingi kuuza hisa zake kwa watanzania - Maxmalipo


  Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr.Donalth Ulomi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza hati iliyopewa kampuni hiyona ambayo inaiwezesha Kampuni kumilikiwa na Umma wa watanzania.

  Akiongea na Wanahabari Dr. Ulomi amesema kwamba Kuanzia Sasa Kampuni ya Maxcom Africa itatambulika kwa Jina la Maxcom Africa Public Limited Company (Maxcom Africa PLC) . Kampuni hii maarufu kwa jina la Maxmalipo ni Moja ya Kampuni zilizoanzishwa na kuendeshwa na wazawa watanzania ambayo imeifikia hatua za Mwisho katika mchakato wa kuanza kuuza hisa zake kwenye soko la hisa. Dr. Olumi amewaambia wanahabari kwamba wanasubiri kibali cha wasimamizi wa Soko la Hisa ili waweze Kuorodhesha Kampuni yao katika Soko hilo

  Kampuni hii ilianzishwa mwaka 2008 na mpaka leo imefika nchi zaidi ya 5 barani Africa.Hafla hiyo ya uzinduzi wa uuzaji wa hisa ulifanyika mapema leo katika makao makuu ya Maxcom Africa Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam.

  Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr. Donalth Ulomi (kulia ) akikata utepe wa kuzindua rasmi Jina Lipya la Kampuni ya Maxcom Africa PLC anayeshuhudia ni Mkurungezi wa Uendeshaji wa Maxcom Africa Bw.Ahmed Lusasi mapema leo katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika makao makuu ya Maxcom Africa PLC Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam.
  Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr,Donalth Ulomi (kulia ) akionesha nembo ya jina jipya Maxcom Africa PLC na kushoto kwake ni Mkurungezi wa Uendeshaji wa Maxcom Africa Bw.Ahmed Lusasi mapema leo katika hafla ya uzinduzi wa Jina jipya la Kampuni hiyo iliyofanyika makao makuu ya Maxcom Africa PLC Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam
  Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr. Donalth Ulomi akifanya mahojiano na mwandishi wa habari mara baada ya uzinduzi rasmi wa Jina Jipya la Kampuni ya Maxcom Africa PLC.

  Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr. Donalth Ulomi akifanya mahojiano na mwandishi wa habari mara baada ya uzinduzi rasmi wa Jina Jipya la Kampuni ya Maxcom Africa PLC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Kampuni ya Wazawa, yakamilisha hatua za Msingi kuuza hisa zake kwa watanzania - Maxmalipo Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top