728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, June 1, 2017

  KAMPUNI YA MAZIWA YA ASAS DAIRIES LTD YANYWESHA MAZIWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI MANISPAA YA IRINGA


  Meneja miradi wa kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Ltd Hassan Swedi akimpa maziwa mlemavu

  Wanafunzi wa shule ya msingi JJ Mungai wakipewa maziwa ya Asas Dairies Ltd leo
  Wafanyakazi wa kampuni ya maziwa ya Asas wakigawa maziwa kwa wanafunzi

  Wanafunzi wa shule ya Msingi Ipogolo wakichukua maziwa

  wanafunzi wakichukua maziwa
  leo siku ya unywaji maziwa duniani
  Wanafunzi wakipewa maziwa kutoka kampuni ya Asas ya mkoani Iringa leo

  Walimu wa shule ya Msingi JJ Mungai wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wwao baada ya kupewa mgao wa maziwa leo

  Wanafunzi wa shule ya Msingi JJ Mungai Iringa mjini wakifurahia maziwa


  wafanyakazi wa kampuni ya Asas wakigawa maziwa kwa wanafunzi leo siku ya unywaji maziwa duniani

  Na MatukiodaimaBlog

  WAKATI leo ni siku ya unywaji maziwa duniani kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Limited imenywesha maziwa wanafunzi zaidi ya 4000 wa shule mbali mbali za Manispaa ya Iringa .

  Shule hizo za msingi zilizopo kanda ya Ruaha ambazo zimeanza kunufaika na unywaji maziwa ,huku walimu wao wakidai baadhi ya wanafunzi wa shule hizo wamekuwa na matokeo mabaya katika mitihani kutokana na unywaji wa pombe ya kienyeji aina ya ulanzi .

  Meneja wa miradi wa kampuni ya Asas Dairies Ltd Hassan Swedi alisema kuwa maadhimisha ya mwaka huu yamelenga zaidi vijana hasa wanafunzi wa shule za msingi mjini Iringa na ndio sababu kampuni yake imelazimika kutoa msaada wa maziwa na majaketi kwa wanafunzi wanaotoka katika familia duni .

  Alisema kuwa kampuni hiyo inaamini kuwa iwapo shule zitaweka utaratibu wa kutoa maziwa kwa wanafunzi afya za wanafunzi hao zitakuwa bora na kiwango cha elimu kinaweza kuongezeka zaidi mashuleni.

  Mbali ya unywaji wa maziwa kuhamasishwa zaidi mashuleni bado viongozi wa serikali wanapaswa kuanza kuhamasha unywaji wa maziwa katika ofisi hizo za umma badala ya kutumia maziwa kutoka nje ya nchi .
  Alisema kuwa kampuni ya Asas Dairies

  Ltd imeendelea kuunga mkono mpango wa lishe mashuleni kama njia ya kuboresha afya na uwezo wa wanafunzi kufanya vizuri kwenye masomo Iringa unazalisha maziwa zaidi ya lita milioni 14 kwa mwaka ila bado kiwanda cha Asas kinasindika lita 400,000 pekee kwa siku .

  Hata hivyo alisema suala la lishe bado ni kikwazo katika mkoa wa Iringa baada ya mkoa huo kuwa mkoa wa pili kwa utapiamlo kitaifa .

  Hivyo alitaka jamii ya wakazi wa mkoa wa Iringa kujenga utamaduni wa kutumia maziwa ili kuongeza lishe na kuwa na afya njema.


  Alisema kuwa mkoa wa Iringa umejipanga kuendelea kuboresha upatikanaji wa maziwa mashuleni kwa kushirikisha wafugaji kama njia ya kukomesha utapiamlo mkubwa mashuleni.


  Kwani alisema kuwa mkoa wa Iringa unapaswa kuondokana na aibu ya utapiamlo kwa watoto na kuwataka wananchi sasa kuanza kuongeza ufugaji wa ng’ombe za maziwa kupitia mradi wa kopa ng’ombe lipa ng’ombe.

  Hata hivyo alipongeza jitihada za kampuni ya maziwa ya Asas kwa kuendelea kuhamasisha unywaji wa maziwa na kuitaka jamii na mkoa wa Iringa kuachana na unywaji wa pombe na badala yake kunywa maziwa zaidi.

  Alisema kuwa mbali ya wanafunzi wa Manispaa ya Iringa kupewa maziwa pia kampuni hiyo imeendesha zoezi kama hilo mkoani Kigoma .

  Mwalimu mkuu msaidizi shule ya Msingi Ipogolo Makrina Mpogole pamoja na kushukuru kampuni ya Asas kwa kutoa maziwa kwa wanafunzi wote shuleni kwake bado alisema kampuni hiyo imetoa msaada wa majacketi kwa wanafunzi wanaotoka familia zisizo na uwezo .

  Mwalimu Mpogole alisema kuwa bado wanaomba wazazi kuangalia uwezekano wa kuwawezesha watoto wao kupata japo paketi moja ya maziwa fresh pindi wanapokwenda shule badala ya wanafunzi hao baadhi yao kunywa pombe aina ya ulanzi .

  Alisema matokeo mabovu kwa baadhi ya wanafunzi yanachangiwa na tabia ya kunywa ulanzi wakiwa mitaaani hivyo iwapo watapewa maziwa yatawasaidia kuongeza afya na kuwa na uwezo zaidi katika masomo .

  Wakati mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi JJ Mungai Haji Mpakati alisema kuwa iwapo utaratibu wa wanafunzi kupewa lishe unaweza kupunguza kiwango cha udumavu na utapiamlo kwa wanafunzi mashule.TAZAMA VIDEO HAPA CHINI

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: KAMPUNI YA MAZIWA YA ASAS DAIRIES LTD YANYWESHA MAZIWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI MANISPAA YA IRINGA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top