728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, June 2, 2017

  EXIM BANK TANZANIA YAPATA TUZO YA BENKI BORA YA MWAKA

   Exim Bank Tanzania imetambuliwa kama Benki bora ya mwaka katika wateja binafsi na biashara ndogondogo na saizi ya kati, yaani ‘Retail banking’ katika tuzo za Banker za Afrika Mashariki zilizofanyika Nairobi, Kenya. 

  Tuzo za Banker za Afrika Mashariki zimedhamiria kuhamasisha ubora kwenye sekta ya fedha katika kanda ya Afrika Mashariki. Kupitia kura 77,000 zilizopigwa na jamii ya sekta ya fedha katika kanda hii benki ya Exim ilichaguliwa kama mshindi wa mwaka huu katika wateja binafsi na biashara ndogo - Retail. 

  Akiongea kwa niaba ya benki hiyo, Mkuu wa kitengo cha fedha Selemani Ponda alisema, “Tunajivunia sana na kushukuru kwa tuzo hii. Tumefanya kazi kubwa kwa muda mrefu kujenga msingi wa kuendeleza operesheni zetu za baadae. Matokeo yanajionyesha, katika miaka ya karibuni amana kutoka kwa wateja wetu imeongezeka na wateja pia wameongezeka. Vilevile faida baada ya kodi imeendelea kukua hadi kufikia kiasi cha shilingi bilioni 72 kwa mwaka 2016.” 

  Ponda ambaye alihudhuria hafla ya tuzo hizo alitoa pongezi kwa waandaaji kwa kuandaa tukio lenye mafanikio kwa miaka mine mfululizo. Hadi sasa tuzo hizo zimevutia ushiriki wa wanataaluma wengi zaidi katika sekta ya benki katika kanda hii. Zaidi ya hapo aliongeza kuwa washirika muhimu kama vile kampuni za teknolojia ambazo husaidia kubadilisha sekta hii pia zilitambuliwa kwa mchango wao. 

  Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi na biashara ndogo Rahul Singh, alisema kuwa uvumbuzi pia umechangia kwa kiasi kikubwa katika kuifanya Exim kuwa benki bora nchini Tanzania na inaheshimika sana katika utoaji huduma na operesheni kupitia jukwaa la kiwango cha juu katika teknolojia. “Uvumbuzi ni ahadi tunayowapa wateja wetu. Benki hii imepata upenyo mkubwa kwa kuweka teknolojia ya viwango vya kimataifa na bidhaa zinazolenga mahitaji ya wateja,” aliongeza.

  Benki ya Exim bank imechukua hatua nyingi katika kitengo hiki ikiwa ni pamoja na kuanzisha huduma ya kipekee inayoitwa "Preferred Banking" ambayo inaruhusu mteja kupata mhudumu wa benki wa kumhudumia, huduma za kipekee katika matawi ya benki, bei upendeleo ya bidhaa na faida za kipekee za kimaisha. Benki ya Exim ilikuwa ndiyo ya kwanza nchini kutambulisha kadi za kimataifa za malipo za MasterCard na Visa Platinum, Tanapa na kadi za Visa za malipo baadaye. Benki hii pia ilianzisha matumizi ya mashine za kutolea fedha yaani ATM na mpango wa mikopo kwa wanawake Tanzania. 

  Juhudi za uanzilishi za Exim zimepitiliza mipaka, mwaka 2007 ilikuwa ni benki ya kwanza kuwa na operesheni nje ya nchi katika nchi ya Comoro. Benki ya Exim pia iliendelea kutanua mbawa zake zaidi katika nchi ya Djibouti Machi 2011, na kuweza kuunganisha kimkakati nchi hizi zilizo katika pembe ya Afrika. Mwaka 2016, Benki ya iliejitanua zaidi kikanda kwa kuwa na matawi matano nchini Uganda. 

  Singh alimalizia kwa kuitambua timu nzima ya benki hiyo haswa wanaotoa huduma moja kwa moja kwa wateja katika matawi ya benki kwa kazi nzuri na kutimiza wajibu wao ipasavyo. Pia aliwashukuru wateja wote wa benki ambao wamechagua kuwa nao na ambao wanaisaidia benki hiyo kuweza kupata mafanikio kwa kuwapa biashara. Benki inajikita kuendeleza mindombinu yake, kuboresha huduma kwa wateja na operesheni ili kutoa huduma za kiwango cha juu kwa wateja. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: EXIM BANK TANZANIA YAPATA TUZO YA BENKI BORA YA MWAKA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top