728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, June 8, 2017

  BALOZI WA BURUNDI NCHINI AKUTANA NA UONGOZI WA EWURA

   Balozi wa Tanzania Nchini Burundi Mheshimiwa Rajabu Hassan Gamaha anayeangalia camera akizungumza na baadhi ya wajumbe wanaoshiriki Mkutano wa 8 wa Afrika Mashariki wa Sekta ya Petroli kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao walifika katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania jijini Bujumbura, Burundi leo kwa mazungumzo yaliyolenga kuimarisha uhusiano mwema ulipo baina ya Burundi na Tanzania. Ujumbe huo uliongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana L. Pallangyo aliyevaa suti nyeupe.

  Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Bwana Felix Ngamlagosi akisisitiza jambo wakati akizungumza na Balozi Rajabu juu ya uhusiano wa Taasisi ya EWURA na Taasisi mpya iliyoanzishwa Nchini Burundi  yenye jukumu la Kudhibiti Nishati ya Mafuta na Maji, pembeni yake ni Mkurugenzi Msaidizi Miundombinu ya Kiuchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhandisi Abdillah Mataka.
  Balozi Rajabu na Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Mazungumzo hayo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: BALOZI WA BURUNDI NCHINI AKUTANA NA UONGOZI WA EWURA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top