728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, May 6, 2017

  WIZARA YA MAMBO YA NJE YAPOKEA MSAADA WA MAGARI KUTOKA OMAN

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) (katikati), akipokea funguo za Magari aina ya Toyota Land Cruiser  kutoka kwa  Balozi wa Omani hapa nchini, Mhe. Ali Abdullah Al Mahruqi. Anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Ramadhan Mwinyi. 

  Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam leo. Baada ya kukabidhiwa magari hayo yenye thamani ya takriban milioni 400 za Tanzania, Waziri Mahiga alisema kuwa msaada huo umetolewa na Serikali ya Oman kwa ajili ya kusaidia masuala ya usafiri katika kipindi hiki cha mpito ambapo Serikali inahamia Dodoma. 
  Waziri Mahiga akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Serikali na Wizara yake kwa ujumla mara baada ya kupokea msaada huo. 
  Waziri akiendelea kuongea huku Watumishi wa Wizara yake wakimsikiliza kwa makini.
  Balozi Al Mahruqi naye akizungumza na kuishukuru Tanzania kwa ushirikiano anaoumpata kwenye utendaji kazi wake hapa nchini. Alisema Serikali yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo huduma za kijamii.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WIZARA YA MAMBO YA NJE YAPOKEA MSAADA WA MAGARI KUTOKA OMAN Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top