728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, May 31, 2017

  wananchi wamekuwa na uelewa wa utekelezaji wa bajeti katika kipaumbele- Tacosode

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  BARAZA la Vyama vya Hiari na Maendeleo ya Jamii (Tacosode) limesema wananchi wamekuwa na uelewa kuhamasisha bajeti kuwa na kipaumbele kwa changamoto zinazowakabili.

  Hayo ameyasema leo Meneja wa Miradi wa Tacosode, Koga Mihama wakati akizungumza waandishi wa habari juu wananchi kuwa na uelewa kuweka umuhimu bajeti katika halmashauri kutatua changamoto zinazowakabili.

  Koga amesema kuwa uelewa huo umetokana na elimu waliopata katika mradi wa uhamasishaji wananchi kushiriki katika masuala ya afya katika kuangalia vipaumbele vya bajeti uliokuwa ukitekelezwa katika Mikoa ya Iringa pamoja na Dodoma.

  Amesema kuwa wananchi mradi huo katika utekezwaji wake katika Halmashauri ya Iringa pamoja na Kongwa mkoani Dodoma wananchi wamekuwa na mwamko katika masuala ya afya ushiriki kwa kuchangia katika huduma za afya.

  Koga amesema kuwa mradi huo ni wa miaka minne lakini umekuwa na matokeo katika wilaya ambazo umetekelezwa kwa wananchi kuwa na mwamko katika masuala ya huduma za afya kwa kuchangia hata nguvu zao pale panapobidi.

  Aidha amesema kuwa mradi huo ukiisha wanaweza kufanya katika sekta zingine ili kuwa maendeleo ya katika masuala mbalimbali kutatuliwa.

  Meneja wa Miradi wa Tacosode, Koga Mihama akizungumza na waandishi wa habari juu ya baraza hilo linavyofanya kazi katika mradi wa afya, leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Afisa Habari,Said Juma na Kushoto ni Afisa mradi wa Tacosode, Nobelrich Ekonea
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: wananchi wamekuwa na uelewa wa utekelezaji wa bajeti katika kipaumbele- Tacosode Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top