728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, May 15, 2017

  WAETHIOPIA ZAIDI YA NANE WAKUTWA WAMEFARIKI PORINI KATIKA KIJIJI CHA AMANI MAKOLO MKOANI RUVUMA

  Ditha nyoni - RUVUMA

  Raia nane kutoka nchi ya Ethiopia wamekutwa wamefariki katika kijiji cha Amani makolo taarafa ya kingonsera wilayani mbinga mkoani wa ruvuma huku wengine 25 wakiwa hai wanashikiriwa na jeshi la polisi.

  Habari kutoka jeshi la polisi mkoa wa ruvuma kupitia kaimu kamanda wa polisi ACP DISAMASI KISUSI zinasema raia hao wa Ethiopia walikuwa wanasafirishwa kwenda nchi ya AFRIKA KUSINI kupitia Upande wa MALAWI mwa ziwa NYASA.

  Vifo vya Waithiopia hao vinatokana na kubebwa kwenye kontena la lori wakitokea NAMANGA, ARUSHWA hivyo kutokana na hali mbaya ya hewa hali zao zilianza kubadilika na kupelekea kufariki.huku miili ya marehemu hao ikiwa imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya MBINGA
  Jeshi la polis mkoa wa ruvuma kwa kushirikiana na jeshi la uhamiaji linaendelea na uchunguzi kubaini walioleta miili ya marehemu na wale wasiliokamatwa hatua za kisheria zitafuatwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAETHIOPIA ZAIDI YA NANE WAKUTWA WAMEFARIKI PORINI KATIKA KIJIJI CHA AMANI MAKOLO MKOANI RUVUMA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top